Deuteronomy 4:7 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Hakuna taifa lolote hata liwe kuu namna gani, ambalo mungu wake yuko karibu nalo, kama alivyo karibu nasi Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, tunapomwomba msaada.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ni taifa gani jingine lililo kubwa kiasi cha kuwa na miungu yao iliyo karibu nao kama Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, alivyo karibu nasi wakati wowote tunapomwomba?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana liko taifa gani kubwa, lililo na Mungu aliye karibu nao, kama Bwana, Mungu wetu, alivyo, kila tumwitapo?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Hakuna taifa lolote hata liwe kuu namna gani, ambalo mungu wake yuko karibu nalo, kama alivyo karibu nasi Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, tunapomwomba msaada.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ni taifa gani jingine lililo kubwa kiasi cha kuwa na miungu yao iliyo karibu nao kama BWANA Mungu wetu alivyo karibu nasi wakati wo wote tunapomwomba?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ni taifa gani jingine lililo kubwa kiasi cha kuwa na miungu yao iliyo karibu nao kama bwana Mwenyezi Mungu wetu alivyo karibu nasi wakati wowote tunapomwomba?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa maana liko taifa gani kubwa, lililo na Mungu aliye karibu nao, kama BWANA Mungu wetu alivyo kila tumwitapo?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Hakuna taifa lolote hata liwe kuu namna gani, ambalo mungu wake yuko karibu nalo, kama alivyo karibu nasi Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, tunapomwomba msaada.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani liko taifa gani kubwa, miungu yake inalolikalia karibu hivi, kama Bwana Mungu wetu alivyo karibu kwetu po pote, tunapomlilia?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana liko taifa gani kubwa, lililo na Mungu aliye karibu nao, kama BWANA, Mungu wetu, alivyo, kila tumwitapo?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Hakuna taifa lolote hata likuwe kubwa namna gani, ambalo mungu wake yuko karibu nalo, kama vile Yawe, Mungu wetu, anavyokuwa karibu nasi tunapomwomba musaada.