Deuteronomy 4:9 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Lakini muwe waangalifu na kujihadhari sana msije mkasahau mambo yale mliyoyaona kwa macho yenu wenyewe. Isije ikatokea hata mara moja maishani mwenu mambo hayo yakasahaulika mioyoni mwenu. Wasimulieni watoto wenu na wajukuu wenu
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwe waangalifu na makini ili msije mkasahau mambo ambayo mliyaona kwa macho yenu, wala kuyaacha yaondoke mioyoni mwenu siku zote za uhai wenu. Mwafundishe hayo watoto wenu na watoto wao baada yao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini, jihadhari nafsi yako, ukailinde roho yako kwa bidii, usije ukayasahau mambo yale uliyoyaona kwa macho yako, yakaondoka moyoni mwako siku zote za maisha yako; bali uwajulishe watoto wako na watoto wa watoto wako;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Lakini muwe waangalifu na kujihadhari sana msije mkasahau mambo yale mliyoyaona kwa macho yenu wenyewe. Isije ikatokea hata mara moja maishani mwenu mambo hayo yakasahaulika mioyoni mwenu. Wasimulieni watoto wenu na wajukuu wenu
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mwe waangalifu, na makini ili msije mkasahau mambo ambayo mliyaona kwa macho yenu, wala kuyaacha yaondoke moyoni mwenu siku zote za uhai wenu. Mwafundishe hayo watoto wenu na watoto wao baada yao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mwe waangalifu, na makini ili msije mkasahau mambo ambayo mliyaona kwa macho yenu, wala kuyaacha yaondoke moyoni mwenu siku zote za uhai wenu. Mwafundishe hayo watoto wenu na watoto wao baada yao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini, jihadhari nafsi yako, ukailinde roho yako kwa bidii, usije ukayasahau mambo yale uliyoyaona kwa macho yako, yakaondoka moyoni mwako siku zote za maisha yako; bali uwajulishe watoto wako na watoto wa watoto wako;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Lakini muwe waangalifu na kujihadhari sana msije mkasahau mambo yale mliyoyaona kwa macho yenu wenyewe. Isije ikatokea hata mara moja maishani mwenu mambo hayo yakasahaulika mioyoni mwenu. Wasimulieni watoto wenu na wajukuu wenu
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Jiangalie tu na kuiangalia roho yako, usiyasahau kabisa hayo mambo, macho yako yaliyoyaona, yasiondoke moyoni mwako siku zote, utakazokuwapo. Nawe uyajulishe kwa wanao na kwa wana wa wanao!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini, jihadhari nafsi yako, ukailinde roho yako kwa bidii, usije ukayasahau mambo yale uliyoyaona kwa macho yako, yakaondoka moyoni mwako siku zote za maisha yako; bali uwajulishe watoto wako na watoto wa watoto wako;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Lakini mukuwe waangalifu na kufanya angalisho sana kusudi musisahau mambo yale muliyoona kwa macho yenu wenyewe, kusudi isitokee hata mara moja katika maisha yenu mambo hayo kusahaulika ndani ya mioyo yenu. Muwaelezee watoto wenu na wajukuu wenu