Deuteronomy 5:14 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
lakini siku ya saba ni siku ya Sabato ambayo imetengwa kwa ajili yangu. Siku hiyo wewe usifanye kazi yoyote, wala mwanao, wala binti yako, wala mtumwa wako wa kiume au wa kike, wala ng'ombe wako, wala punda wako, wala mnyama wako yeyote, wala mgeni aliye ndani ya malango yako, ili mtumwa wako wa kiume na wa kike wapate kupumzika vilevile kama wewe.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini siku ya saba ni Sabato kwa Mwenyezi Mungu, Mungu wako. Siku hiyo hutafanya kazi yoyote, wewe, wala mwanao au binti yako, wala mtumishi wa kiume au wa kike, wala ng’ombe wako, punda wako au mnyama wako yeyote, wala mgeni aliye malangoni mwako, ili mtumishi wako wa kiume na wa kike wapate kupumzika kama wewe.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
lakini siku ya saba ni Sabato ya Bwana, Mungu wako; siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwanao, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala ng'ombe wako, wala punda wako, wala mnyama wako ye yote, wala mgeni aliye ndani ya malango yako, ili mtumwa wako na mjakazi wako wapumzike vile vile kama wewe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
lakini siku ya saba ni siku ya Sabato ambayo imetengwa kwa ajili yangu. Siku hiyo wewe usifanye kazi yoyote, wala mwanao, wala binti yako, wala mtumwa wako wa kiume au wa kike, wala ng'ombe wako, wala punda wako, wala mnyama wako yeyote, wala mgeni aliye ndani ya malango yako, ili mtumwa wako wa kiume na wa kike wapate kupumzika vilevile kama wewe.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini siku ya Saba ni Sabato kwa BWANA, Mungu wako. Siku hiyo hutafanya kazi yo yote, ikiwa ni wewe, wala mwanao au binti yako, wala mtumishi wa kiume au mtumishi wa kike, wala ng'ombe wako, punda wako au mnyama wako ye yote, wala mgeni aliyeko malangoni mwako, ili kwamba mtumishi wako wa kiume na wa kike wapate kumpumzika kama wewe.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini siku ya Saba ni Sabato kwa bwana, Mungu wako. Siku hiyo hutafanya kazi yoyote, wewe, wala mwanao au binti yako, wala mtumishi wa kiume au mtumishi wa kike, wala ng’ombe wako, punda wako au mnyama wako yeyote, wala mgeni aliyeko malangoni mwako, ili kwamba mtumishi wako wa kiume na wa kike wapate kupumzika kama wewe.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
lakini siku ya saba ni Sabato ya BWANA, Mungu wako; siku hiyo usifanye kazi yoyote, wewe, wala mwanao, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala ng'ombe wako, wala punda wako, wala mnyama wako yeyote, wala mgeni aliye ndani ya malango yako, ili mtumwa wako na mjakazi wako wapumzike vile vile kama wewe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
lakini siku ya saba ni siku ya Sabato ambayo imetengwa kwa ajili yangu. Siku hiyo wewe usifanye kazi yoyote, wala mwanao, wala binti yako, wala mtumwa wako wa kiume au wa kike, wala ng'ombe wako, wala punda wako, wala mnyama wako yeyote, wala mgeni aliye ndani ya malango yako, ili mtumwa wako wa kiume na wa kike wapate kupumzika vilevile kama wewe.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini siku ya saba ndiyo ya kumpumzikia Bwana Mungu wako. Hapo usifanye kazi yo yote, wala wewe, wala mwanao wa kiume, wala wa kike, wala mtumishi wako wa kiume, wala wa kike, wala ng'ombe wako wala punda wako wala nyama wako ye yote wa kufuga, wala mgeni wako aliomo malangoni mwako, mtumishi wako wa kiume na wa kike apate kupumzika kama wewe!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
lakini siku ya saba ni Sabato ya BWANA, Mungu wako; siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwanao, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala ng’ombe wako, wala punda wako, wala mnyama wako ye yote, wala mgeni aliye ndani ya malango yako, ili mtumwa wako na mjakazi wako wapumzike vile vile kama wewe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini siku ya saba ni Sabato ya Yawe, Mungu wako. Siku hiyo usifanye kazi yoyote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mutumwa wako, wala mujakazi wako, wala ngombe wako, wala punda wako, wala nyama wako yeyote, wala mugeni anayekuwa katika nyumba yako, kusudi mutumwa wako na mujakazi wako wapate kupumzika vilevile kama vile wewe.