Deuteronomy 5:16 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“ ‘Waheshimu baba yako na mama yako, kama vile mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako nilivyokuamuru; fanya hivyo ili uishi siku nyingi na kufanikiwa katika nchi ambayo ninakupatia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Waheshimu baba yako na mama yako, kama Mwenyezi Mungu, Mungu wako, alivyokuagiza, ili siku zako zipate kuwa nyingi na kufanikiwa katika nchi Mwenyezi Mungu, Mungu wako, anayokupa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Waheshimu baba yako na mama yako; kama Bwana, Mungu wako, alivyokuamuru, siku zako zipate kuzidi, nawe upate kufanikiwa katika nchi upewayo na Bwana, Mungu wako.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“‘Waheshimu baba yako na mama yako, kama vile mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako nilivyokuamuru; fanya hivyo ili uishi siku nyingi na kufanikiwa katika nchi ambayo ninakupatia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Waheshimu baba yako na mama yako, kama BWANA Mungu wako alivyokuagiza, ili siku zako zipate kuwa nyingi na kufanikiwa katika nchi BWANA Mungu wako anayokupa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Waheshimu baba yako na mama yako, kama bwana Mwenyezi Mungu wako alivyokuagiza, ili siku zako zipate kuwa nyingi na kufanikiwa katika nchi bwana Mwenyezi Mungu wako anayokupa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Waheshimu baba yako na mama yako; kama BWANA, Mungu wako, alivyokuamuru, siku zako zipate kuzidi, nawe upate kufanikiwa katika nchi upewayo na BWANA, Mungu wako.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“ ‘Waheshimu baba yako na mama yako, kama vile mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako nilivyokuamuru; fanya hivyo ili uishi siku nyingi na kufanikiwa katika nchi ambayo ninakupatia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mheshimu baba yako na mama yako, kama Bwana Mungu wako alivyokuagiza, siku zako zipate kuwa nyingi, nawe upate kuona mema katika nchi, akupayo Bwana Mungu wako!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Waheshimu baba yako na mama yako; kama BWANA, Mungu wako, alivyokuamuru, siku zako zipate kuzidi, nawe upate kufanikiwa katika nchi upewayo na BWANA, Mungu wako.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Uheshimu baba yako na mama yako, kama vile mimi Yawe, Mungu wako, nilivyokuamuru, kusudi uishi maisha marefu na kufanikiwa katika inchi ninayokupatia mimi Yawe, Mungu wako.