Deuteronomy 5:22 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Hizi ndizo amri Mwenyezi-Mungu alizowaambieni nyote kwa sauti kubwa kutoka katika moto na lile wingu zito na giza nene. Aliwaambieni mlipokuwa mmekusanyika kule mlimani na hakuongeza hapo amri nyingine. Kisha akaziandika juu ya vibao viwili vya mawe, akanipatia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hizi ndizo amri alizozitangaza Mwenyezi Mungu kwa sauti kubwa kwa kusanyiko lenu lote huko mlimani kutoka kati ya moto na wingu na giza nene, wala hakuongeza chochote zaidi. Kisha akaziandika juu ya vibao viwili vya mawe, naye akanipa mimi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Haya ndiyo maneno ambayo Bwana aliwaambia mkutano wenu wote mlimani kwa sauti kuu toka kati ya moto, na wingu, na giza kuu; wala hakuongeza neno. Akayaandika juu ya mbao mbili za mawe, akanipa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Hizi ndizo amri Mwenyezi-Mungu alizowaambieni nyote kwa sauti kubwa kutoka katika moto na lile wingu zito na giza nene. Aliwaambieni mlipokuwa mmekusanyika kule mlimani na hakuongeza hapo amri nyingine. Kisha akaziandika juu ya vibao viwili vya mawe, akanipatia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hizi ndizo amri alizozitangaza BWANA kwa sauti kubwa kwa kusanyiko lenu lote huko mlimani kutoka kwenye moto, wingu na giza nene, wala hakuongeza cho chote zaidi. Kisha akaziandika juu ya vibao viwili vya mawe, naye akanipa mimi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hizi ndizo amri alizozitangaza bwana kwa sauti kubwa kwa kusanyiko lenu lote huko mlimani kutoka kwenye moto, wingu na giza nene, wala hakuongeza chochote zaidi. Kisha akaziandika juu ya vibao viwili vya mawe, naye akanipa mimi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Haya ndiyo maneno ambayo BWANA aliwaambia mkutano wenu wote mlimani kwa sauti kuu toka kati ya moto, na wingu, na giza kuu; wala hakuongeza neno. Akayaandika juu ya mbao mbili za mawe, akanipa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Hizi ndizo amri Mwenyezi-Mungu alizowaambieni nyote kwa sauti kubwa kutoka katika moto na lile wingu zito na giza nene. Aliwaambieni mlipokuwa mmekusanyika kule mlimani na hakuongeza hapo amri nyingine. Kisha akaziandika juu ya vibao viwili vya mawe, akanipatia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Maneno haya Bwana aliwaambia wao wote wa mkutano wenu kule mlimani kwa sauti kuu toka motoni mle winguni mwenye weusi, hakuongeza neno, kisha akayaandika katika mbao mbili za mawe, akanipa mimi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Haya ndiyo maneno ambayo BWANA aliwaambia mkutano wenu wote mlimani kwa sauti kuu toka kati ya moto, na wingu, na giza kuu; wala hakuongeza neno. Akayaandika juu ya mbao mbili za mawe, akanipa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Hizi ndizo amri Yawe alizowaambia ninyi wote kwa sauti kubwa kutoka katika moto na lile wingu zito na giza nene, mulipokuwa mumekusanyika kule kwenye mulima. Hakuongeza hapo amri ingine. Kisha akaandika juu ya vibao viwili vya mawe, akanipatia.