Deuteronomy 5:33 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mtafuata njia yote Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, aliyowaamuru kufuata ili mambo yenu yawaendee vyema na mpate kuishi muda mrefu katika nchi mtakayotwaa iwe mali yenu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Fuateni yale yote ambayo Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, aliwaagiza, ili mpate kuishi, kustawi na kuziongeza siku zenu katika nchi mtakayoimiliki.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Endeni njia yote aliyowaagiza Bwana, Mungu wenu, mpate kuwa hai, na kufanikiwa, mkafanye siku zenu kuwa nyingi katika nchi mtakayoimiliki.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mtafuata njia yote Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, aliyowaamuru kufuata ili mambo yenu yawaendee vyema na mpate kuishi muda mrefu katika nchi mtakayotwaa iwe mali yenu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Fuateni yale yote ambayo BWANA Mungu wenu aliwaagiza, ili mpate kuishi, kustawi na kuziongeza siku zenu katika nchi mtakayoimiliki.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Fuateni yale yote ambayo bwana Mwenyezi Mungu wenu aliwaagiza, ili mpate kuishi, kustawi na kuziongeza siku zenu katika nchi mtakayoimiliki.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nendeni njia yote aliyowaagiza BWANA, Mungu wenu, mpate kuwa hai, na kufanikiwa, mkafanye siku zenu kuwa nyingi katika nchi mtakayoimiliki.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mtafuata njia yote Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, aliyowaamuru kufuata ili mambo yenu yawaendee vyema na mpate kuishi muda mrefu katika nchi mtakayotwaa iwe mali yenu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ila njia zote, Bwana Mungu wenu alizowaagiza ninyi, zishikeni na kuzifuata, mkae uzimani na kuona mema, nazo siku zenu ziwe nyingi katika nchi, mnayokwenda kuichukua, iwe yenu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Endeni njia yote aliyowaagiza BWANA, Mungu wenu, mpate kuwa hai, na kufanikiwa, mkafanye siku zenu kuwa nyingi katika nchi mtakayoimiliki.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mutafuata njia yote Yawe, Mungu wenu, aliyowaamuru kufuata kusudi mambo yenu yawaendekee vizuri na mupate kuishi muda murefu katika inchi mutakayotwaa ikuwe mali yenu.