Deuteronomy 6:24 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, Mwenyezi-Mungu alituamuru kuzitii kanuni hizi zote na kumcha kwa faida yetu wenyewe; apate kutulinda daima kama hivi leo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwenyezi Mungu akatuagiza tutii amri hizi zote na kumcha Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, ili tupate kustawi na kuendelea kuwa hai kama ilivyo leo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana akatuamuru kuzifanya amri hizi zote, tumche Bwana, Mungu wetu, tuone mema sikuzote ili atuhifadhi hai kama hivi leo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, Mwenyezi-Mungu alituamuru kuzitii kanuni hizi zote na kumcha kwa faida yetu wenyewe; apate kutulinda daima kama hivi leo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
BWANA akatuagiza tutii amri hizi zote na kumcha BWANA Mungu wetu, ili tupate kustawi na kuendelea kuwa hai kama ilivyo leo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
bwana akatuagiza tutii amri hizi zote na kumcha bwana Mwenyezi Mungu wetu, ili tupate kustawi na kuendelea kuwa hai kama ilivyo leo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
BWANA akatuamuru kuzifanya amri hizi zote, tumche BWANA, Mungu wetu, tuone mema siku zote ili atuhifadhi hai kama hivi leo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, Mwenyezi-Mungu alituamuru kuzitii kanuni hizi zote na kumcha kwa faida yetu wenyewe; apate kutulinda daima kama hivi leo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, Bwana alipotuagiza kuyafanya haya maongozi yote kwa kumcha Bwana Mungu wetu, tuone mema siku zote za maisha yetu, kama inavyoelekea leo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
BWANA akatuamuru kuzifanya amri hizi zote, tumche BWANA, Mungu wetu, tuone mema sikuzote ili atuhifadhi hai kama hivi leo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, Yawe akatuamuru kutii masharti haya yote na kumwogopa kwa faida yetu wenyewe, apate kutulinda siku zote kama hivi leo.