Deuteronomy 7:12 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Mkisikiliza maagizo haya na kuyashika hata kuyatenda, Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, atashika agano lake nanyi na atawaonesheni fadhili kama alivyowaahidi babu zenu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mkizingatia sheria hizi na kuzifuata kwa uangalifu, basi Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, atatunza agano lake la upendo nanyi, kama alivyowaapia baba zenu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na itakuwa, kwa sababu mwazisikiliza hukumu hizi, na kuzishika na kuzitenda, basi Bwana, Mungu wako, atakutimilizia agano na rehema aliyowaapia baba zako;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Mkisikiliza maagizo haya na kuyashika hata kuyatenda, Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, atashika agano lake nanyi na atawaonesheni fadhili kama alivyowaahidi babu zenu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kama mkizingatia sheria hizi na kuzifuata kwa uangalifu, basi BWANA Mungu wenu atatunza Agano lake la upendo nanyi, kama alivyowaapia baba zenu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kama mkizingatia sheria hizi na kuzifuata kwa uangalifu, basi bwana Mwenyezi Mungu wenu atatunza Agano lake la upendo nanyi, kama alivyowaapia baba zenu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na itakuwa, kwa sababu mnazisikiliza hukumu hizi, na kuzishika na kuzitenda, basi BWANA, Mungu wako, atakutimilizia agano na rehema aliyowaapia baba zako;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Mkisikiliza maagizo haya na kuyashika hata kuyatenda, Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, atashika agano lake nanyi na atawaonesheni fadhili kama alivyowaahidi babu zenu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Itakuwa, mtakapoyasikia haya maamuzi na kuyaangalia, myafanye, naye Bwana Mungu wako atakutimilizia maagano na magawio, aliyowaapia baba zako.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na itakuwa, kwa sababu mwazisikiliza hukumu hizi, na kuzishika na kuzitenda, basi BWANA, Mungu wako, atakutimilizia agano na rehema aliyowaapia baba zako;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Mukisikiliza maagizo haya na kuyashika hata kuyatenda, Yawe, Mungu wenu, atashika agano lake nanyi na kuwatendea mema kama vile alivyowaahidi babu zenu.