Deuteronomy 7:13 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Atawapenda na kuwabariki, nanyi mtaongezeka na kuwa na wazawa wengi; atayabariki mashamba yenu ili mpate nafaka, divai na mafuta; atawabariki kwa kuwapeni ng'ombe na kondoo wengi katika nchi aliyowaahidi babu zenu kuwa atawapeni nyinyi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Atawapenda ninyi na kuwabariki na kuongeza idadi yenu. Atabariki uzao wa tumbo lenu, mazao ya nchi yenu, nafaka, divai mpya na mafuta, ndama za ng’ombe wa makundi yenu, na kondoo wa makundi yenu katika nchi ile aliyoapa kuwapa baba zenu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
naye atakupenda na kukubarikia na kukuongeza tena ataubarikia uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, nafaka zako na divai yako, na mafuta yako, maongeo ya ng'ombe zako, na wadogo wa kondoo zako, katika nchi aliyowaapia baba zako kuwa atakupa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Atawapenda na kuwabariki, nanyi mtaongezeka na kuwa na wazawa wengi; atayabariki mashamba yenu ili mpate nafaka, divai na mafuta; atawabariki kwa kuwapeni ng'ombe na kondoo wengi katika nchi aliyowaahidi babu zenu kuwa atawapeni nyinyi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Atawapenda ninyi na kuwabariki na kuongeza idadi yenu. Atabariki uzao wa tumbo lenu, mazao ya nchi yenu, nafaka, divai mpya na mafuta, ndama wa ng'ombe wa kundi lenu na kondoo za kundi lenu katika nchi ile aliyoapa kuwapa baba zenu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Atawapenda ninyi na kuwabariki na kuongeza idadi yenu. Atabariki uzao wa tumbo lenu, mazao ya nchi yenu, nafaka, divai mpya na mafuta, ndama za ng’ombe wa makundi yenu, na kondoo za makundi yenu katika nchi ile aliyoapa kuwapa baba zenu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
naye atakupenda na kukubariki na kukuongeza tena ataubariki uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, nafaka zako na divai yako, na mafuta yako, kuongezeka kwa ng'ombe na kondoo wako, katika nchi aliyowaapia baba zako kuwa atakupa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Atawapenda na kuwabariki, nanyi mtaongezeka na kuwa na wazawa wengi; atayabariki mashamba yenu ili mpate nafaka, divai na mafuta; atawabariki kwa kuwapeni ng'ombe na kondoo wengi katika nchi aliyowaahidi babu zenu kuwa atawapeni nyinyi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, atakapokupenda, akubariki na kukufanya kuwa wengi, ayabariki nayo mazao ya tumbo lako nayo mazao ya shamba lako, ngano zako na mvinyo zako mbichi na mafuta yako na ndama wako na wana kondoo wako, watakaozaliwa katika nchi hiyo, Bwana aliyowaapia baba zako kukupa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
naye atakupenda na kukubarikia na kukuongeza tena ataubarikia uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, nafaka zako na divai yako, na mafuta yako, maongeo ya ng’ombe zako, na wadogo wa kondoo zako, katika nchi aliyowaapia baba zako kuwa atakupa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Atawapenda na kuwabariki, nanyi mutaongezeka na kuwa na wazao wengi. Atabariki mashamba yenu kusudi mupate ngano, divai na mafuta. Atawabariki kwa kuwapa ngombe na kondoo wengi katika inchi aliyowaahidi babu zenu kwamba atawapa ninyi.