Deuteronomy 7:16 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Angamizeni taifa lolote ambalo Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu; atalitia mikononi mwenu, wala msilionee huruma. Msiabudu miungu yao, kwani jambo hili litakuwa mtego kwenu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ni lazima mwangamize watu wote ambao Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, atawatia mikononi mwenu. Msiwatazame kwa kuwahurumia na msiitumikie miungu yao, kwa kuwa itakuwa mtego kwenu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nawe angamiza mataifa yote atakayokupa Bwana, Mungu wako; jicho lako lisiwahurumie, wala usiitumikie miungu yao; kwani litakuwa ni mtego kwako jambo hilo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Angamizeni taifa lolote ambalo Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu; atalitia mikononi mwenu, wala msilionee huruma. Msiabudu miungu yao, kwani jambo hili litakuwa mtego kwenu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ni lazima mwangamize watu wote ambao BWANA Mungu wenu atawatia mikononi mwenu. Msiwatazame kwa kuwahurumia na msitumikie miungu yao, kwa kuwa itakuwa mtego kwenu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ni lazima mwangamize watu wote ambao bwana Mwenyezi Mungu wenu atawatia mikononi mwenu. Msiwatazame kwa kuwahurumia na msiitumikie miungu yao, kwa kuwa itakuwa mtego kwenu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nawe angamiza mataifa yote atakayokupa BWANA, Mungu wako; jicho lako lisiwahurumie, wala usiitumikie miungu yao; kwani jambo hilo litakuwa ni mtego kwako.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Angamizeni taifa lolote ambalo Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu; atalitia mikononi mwenu, wala msilionee huruma. Msiabudu miungu yao, kwani jambo hili litakuwa mtego kwenu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nayo makabila yote, Bwana Mungu wako atakayokupa, uyale, usiyaonee huruma kabisa, wala usiitumikie miungu yao, kwani hii itakuwa tanzi la kukunasa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nawe angamiza mataifa yote atakayokupa BWANA, Mungu wako; jicho lako lisiwahurumie, wala usiitumikie miungu yao; kwani litakuwa ni mtego kwako jambo hilo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Muangamize taifa lolote ambalo Yawe, Mungu wenu atalitia katika mikono yenu, wala musilionee huruma. Musiabudu miungu yao, maana jambo hili litakuwa mutego kwenu.