Deuteronomy 7:19 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kumbukeni maradhi mabaya mliyoyaona kwa macho yenu, miujiza na maajabu na nguvu kubwa na uwezo mkuu, ambavyo Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu; alitumia kuwakomboa; hivyo ndivyo atakavyowatenda watu mnaowaogopa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mliona kwa macho yenu wenyewe majaribu makubwa, ishara za miujiza na maajabu, mkono wenye nguvu na ulionyooshwa, ambao kwa huo Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, aliwatoa mtoke Misri. Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, atawafanyia hivyo watu wote ambao mnawaogopa sasa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
uyakumbuke hayo majaribu makuu yaliyoyaona macho yako, na hizo ishara, na maajabu, na mkono wa nguvu, na mkono ulionyoka, aliokutolea nje Bwana, Mungu wako; ndivyo atakavyowafanya Bwana, Mungu wako, mataifa yote unaowaogopa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kumbukeni maradhi mabaya mliyoyaona kwa macho yenu, miujiza na maajabu na nguvu kubwa na uwezo mkuu, ambavyo Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu; alitumia kuwakomboa; hivyo ndivyo atakavyowatenda watu mnaowaogopa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mliona kwa macho yenu wenyewe majaribu makubwa, ishara za miujiza na maajabu, mkono wenye nguvu na ulionyooshwa, ambao kwa huo BWANA Mungu wenu aliwatoa mtoke Misri. BWANA Mungu wenu atawafanyia hivyo watu wote ambao mnawaogopa sasa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mliona kwa macho yenu wenyewe majaribu makubwa, ishara za miujiza na maajabu, mkono wenye nguvu na ulionyooshwa, ambao kwa huo bwana Mwenyezi Mungu wenu aliwatoa mtoke Misri. bwana Mwenyezi Mungu wenu atawafanyia hivyo watu wote ambao mnawaogopa sasa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
uyakumbuke hayo majaribu makuu yaliyoyaona macho yako, na hizo ishara, na maajabu, na mkono wa nguvu, na mkono ulionyoka, aliokutolea nje BWANA, Mungu wako; ndivyo atakavyowafanya BWANA, Mungu wako, mataifa yote unaowaogopa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kumbukeni maradhi mabaya mliyoyaona kwa macho yenu, miujiza na maajabu na nguvu kubwa na uwezo mkuu, ambavyo Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu; alitumia kuwakomboa; hivyo ndivyo atakavyowatenda watu mnaowaogopa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yakumbuke hayo majaribu makuu, macho yako yaliyoyaona, navyo vielekezo na vioja, nacho kiganja chake chenye nguvu, nao mkono, Bwana Mungu wako alioukunjua alipokutoa. Hivyo ndivyo, Bwana Mungu wako atakavyoyafanyizia makabila yote, wewe unayoyaogopa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
uyakumbuke hayo majaribu makuu yaliyoyaona macho yako, na hizo ishara, na maajabu, na mkono wa nguvu, na mkono ulionyoka, aliokutolea nje BWANA, Mungu wako; ndivyo atakavyowafanya BWANA, Mungu wako, mataifa yote unaowaogopa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mukumbuke ugonjwa mukali muliouona kwa macho yenu, miujiza na maajabu na nguvu kubwa na uwezo mukubwa, ambavyo Yawe, Mungu wenu alitumia kwa kuwakomboa; vile ndivyo atakavyowatendea watu munaowaogopa.