Deuteronomy 7:2 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Pia, baada ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, kuyatia mikononi mwenu, mkawashinda watu hao na kuwaangamiza kabisa, msifanye agano lolote nao wala msiwahurumie.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
pia Mwenyezi Mungu, Mungu wako, atakapowatia mkononi mwako na ukawashinda, basi ni lazima uwaangamize wote kabisa. Usifanye agano nao, wala usiwahurumie.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
wakati Bwana, Mungu wako, atakapowatoa mbele yako, nawe utawapiga; wakati huo ndipo uwaondoe kabisa; usifanye agano nao, wala kuwahurumia; wala usioane nao;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Pia, baada ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, kuyatia mikononi mwenu, mkawashinda watu hao na kuwaangamiza kabisa, msifanye agano lolote nao wala msiwahurumie.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
pia BWANA Mungu wako atakapowatia mkononi mwako na ukawashinda, basi ni lazima uwaangamize wote kabisa. Usifanye agano nao, usiwahurumie.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
pia bwana Mwenyezi Mungu wako atakapowatia mkononi mwako na ukawashinda, basi ni lazima uwaangamize wote kabisa. Usifanye agano nao, wala usiwahurumie.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
wakati BWANA, Mungu wako, atakapowatoa mbele yako, nawe utawapiga; wakati huo ndipo uwaondoe kabisa; usifanye agano nao, wala kuwahurumia; wala usioane nao;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Pia, baada ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, kuyatia mikononi mwenu, mkawashinda watu hao na kuwaangamiza kabisa, msifanye agano lolote nao wala msiwahurumie.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Bwana Mungu wako atakapowatoa mbele yako, uwapige, sharti uwatie mwiko kabisa wa kuwapo, usifanye agano nao, wala usiwahurumie.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
wakati BWANA, Mungu wako, atakapowatoa mbele yako, nawe utawapiga; wakati huo ndipo uwaondoe kabisa; usifanye agano nao, wala kuwahurumia; wala usioane nao;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Vilevile, kisha Yawe, Mungu wenu, kuyatia katika mikono yenu, mutayashinda na kuyaangamiza kabisa. Musifanye agano lolote nayo wala musiyahurumie.