Deuteronomy 7:25 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Teketezeni kwa moto sanamu zao za kuchonga za miungu yao. Msitamani fedha wala dhahabu yao, wala msiichukue na kuifanya mali yenu. Kufanya hivyo ni mtego kwenu na ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Sanamu za miungu yao mtazichoma moto. Msitamani fedha wala dhahabu iliyo juu ya vinyago hivyo, wala msiichukue iwe yenu, la sivyo mtakuwa mmetekwa nayo. Kwa kuwa ni chukizo kwa Mwenyezi Mungu, Mungu wenu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Sanamu za kuchonga za miungu yao mtaziteketeza kwa moto; usitamani fedha wala dhahabu iliyo juu yao, wala usiitwae iwe yako usije ukanaswa nayo; kwa maana ni machukizo kwa Bwana, Mungu wako;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Teketezeni kwa moto sanamu zao za kuchonga za miungu yao. Msitamani fedha wala dhahabu yao, wala msiichukue na kuifanya mali yenu. Kufanya hivyo ni mtego kwenu na ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Vinyago vya miungu yao mtavichoma moto. Msitamani fedha wala dhahabu iliyo juu yao, wala msizichukue kwa ajili yenu, la sivyo mtakuwa mmetekwa navyo. Kwa kuwa ni chukizo kwa BWANA Mungu wenu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Vinyago vya miungu yao mtavichoma moto. Msitamani fedha wala dhahabu iliyo juu yao, wala msizichukue kwa ajili yenu, la sivyo mtakuwa mmetekwa navyo. Kwa kuwa ni chukizo kwa bwana Mwenyezi Mungu wenu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Sanamu za kuchonga za miungu yao mtaziteketeza kwa moto; usitamani fedha wala dhahabu iliyo juu yao, wala usiitwae iwe yako usije ukanaswa nayo; kwa maana ni machukizo kwa BWANA, Mungu wako;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Teketezeni kwa moto sanamu zao za kuchonga za miungu yao. Msitamani fedha wala dhahabu yao, wala msiichukue na kuifanya mali yenu. Kufanya hivyo ni mtego kwenu na ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Vinyago vya miungu yao vya kuchongwa sharti mviteketeze kwa moto, usitamani kuzichukua fedha na dhahabu vilizotiwa, usinaswe nazo, kwani zinamchukiza Bwana Mungu wako.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Sanamu za kuchonga za miungu yao mtaziteketeza kwa moto; usitamani fedha wala dhahabu iliyo juu yao, wala usiitwae iwe yako usije ukanaswa nayo; kwa maana ni machukizo kwa BWANA, Mungu wako;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Muteketeze kwa moto sanamu za miungu yao. Musitamani feza wala zahabu yao, wala musiitwae na kuifanya mali yenu. Kufanya hivyo ni mutego kwenu na ni chukizo kwa Yawe, Mungu wenu.