Deuteronomy 7:4 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mkifanya hivyo wao watawapotosha watoto wenu wasimfuate Mwenyezi-Mungu, na kuwafanya waabudu miungu mingine, nayo hasira ya Mwenyezi-Mungu itawaka juu yenu, halafu atawaangamiza mara moja.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa maana watamgeuza mwanao aache kunifuata, ili aitumikia miungu mingine, nayo hasira ya Mwenyezi Mungu itawaka dhidi yako, naye atakuangamiza ghafula.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa kuwa atamkengeusha mwanao mume asinifuate, ili wapate kuabudu miungu mingine; ndipo itakapowaka hasira ya Bwana juu yenu, naye atakuangamiza upesi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mkifanya hivyo wao watawapotosha watoto wenu wasimfuate Mwenyezi-Mungu, na kuwafanya waabudu miungu mingine, nayo hasira ya Mwenyezi-Mungu itawaka juu yenu, halafu atawaangamiza mara moja.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa maana watamgeuza mwanao aache kunifuata, ili aitumikia miungu mingine, nayo hasira ya BWANA itawaka dhidi yako, naye atakuangamiza ghafula.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa maana watamgeuza mwanao aache kunifuata, ili aitumikia miungu mingine, nayo hasira ya bwana itawaka dhidi yako, naye atakuangamiza ghafula.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa kuwa atamkengeusha mwanao asinifuate, ili wapate kuabudu miungu mingine; ndipo itakapowaka hasira ya BWANA juu yenu, naye atakuangamiza upesi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mkifanya hivyo wao watawapotosha watoto wenu wasimfuate Mwenyezi-Mungu, na kuwafanya waabudu miungu mingine, nayo hasira ya Mwenyezi-Mungu itawaka juu yenu, halafu atawaangamiza mara moja.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani ataugeuza moyo wa mwanao, aache kunifuata, watumikie miungu mingine; ndipo, makali ya Bwana yatakapokuwakia, akuangamize upesi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa kuwa atamkengeusha mwanao mume asinifuate, ili wapate kuabudu miungu mingine; ndipo itakapowaka hasira ya BWANA juu yenu, naye atakuangamiza upesi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mukifanya hivyo wao watawapotosha watoto wenu wasimufuate Yawe, na kuwafanya waabudu miungu mingine, nayo hasira ya Yawe itawaka juu yenu, halafu atawaangamiza mara moja.