Deuteronomy 7:5 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini watendeni hivi: Mtazivunjilia mbali madhabahu zao na kuzibomoa nguzo zao. Na sanamu za Ashera mtazikatilia mbali na kuzitia moto sanamu zao za kuchonga.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hili ndilo utakalowafanyia: Vunja madhabahu yao, vunja mawe yao ya kuabudia, katakata nguzo zao za Ashera, na kuchoma sanamu zao kwa moto;
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini watendeni hivi; zivunjeni madhabahu zao zibomosheni nguzo zao, yakateni maashera yao, ziteketezeni kwa moto sanamu zao za kuchonga.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini watendeni hivi: Mtazivunjilia mbali madhabahu zao na kuzibomoa nguzo zao. Na sanamu za Ashera mtazikatilia mbali na kuzitia moto sanamu zao za kuchonga.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hili ndilo utakalowafanyia: Vunja madhabahu zao, yabomoe mawe yao yaliyowekwa wakfu, katakata nguzo zao za Ashera na kuchoma sanamu zao kwa moto.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hili ndilo utakalowafanyia: Vunja madhabahu yao, vunja mawe yao ya kuabudia, katakata nguzo zao za Ashera na kuchoma sanamu zao kwa moto.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini watendeni hivi; zivunjeni madhabahu zao zibomoeni nguzo zao, yakateni maashera yao, ziteketezeni kwa moto sanamu zao za kuchonga.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini watendeni hivi: Mtazivunjilia mbali madhabahu zao na kuzibomoa nguzo zao. Na sanamu za Ashera mtazikatilia mbali na kuzitia moto sanamu zao za kuchonga.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ila mwafanyizie hivyo: pao pa kutambikia sharti mpabomoe, nazo nguzo zao za mawe za kutambikia mzivunje, nayo miti yao ya Ashera mwikate, navyo vinyago vyao vya kuchongwa mviteketeze kwa moto.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini watendeni hivi; zivunjeni madhabahu zao zibomosheni nguzo zao, yakateni maashera yao, ziteketezeni kwa moto sanamu zao za kuchonga.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini muwatendee hivi: Mutavunja mazabahu zao na kubomoa nguzo zao. Na sanamu za Ashera mutakata na kuchoma sanamu zao za kuchonga.