Deuteronomy 7:8 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini ni kwa sababu Mwenyezi-Mungu anawapenda na anashika kiapo alichowaapia babu zenu, ndiyo maana aliwaokoeni kwa mkono wake wenye nguvu na kuwaokoa toka utumwani, toka mikono ya Farao mfalme wa Misri.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini ni kwa sababu Mwenyezi Mungu aliwapenda ninyi na kutunza kiapo alichowaapia babu zenu kwamba atawatoa ninyi kwa mkono wenye nguvu na kuwakomboa kutoka nchi ya utumwa, kutoka nguvu za Farao mfalme wa Misri.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
bali kwa sababu Bwana anawapenda, na kwa sababu alitaka kuutimiza uapo wake aliowaapia baba zenu, ndiyo sababu Bwana akawatoa kwa mkono wa nguvu, akawakomboa katika nyumba ya utumwa, katika mkono wa Farao, mfalme wa Misri.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini ni kwa sababu Mwenyezi-Mungu anawapenda na anashika kiapo alichowaapia babu zenu, ndiyo maana aliwaokoeni kwa mkono wake wenye nguvu na kuwaokoa toka utumwani, toka mikono ya Farao mfalme wa Misri.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini ni kwa sababu BWANA aliwapenda ninyi na kutunza kiapo alichowaapia babu zenu kwamba atawatoa ninyi kwa mkono wenye nguvu na kuwakomboa kutoka nchi ya utumwa, kutoka nguvu za Farao mfalme wa Misri.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini ni kwa sababu bwana aliwapenda ninyi na kutunza kiapo alichowaapia babu zenu kwamba atawatoa ninyi kwa mkono wenye nguvu na kuwakomboa kutoka nchi ya utumwa, kutoka nguvu za Farao mfalme wa Misri.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
bali kwa sababu BWANA anawapenda, na kwa sababu alitaka kukitimiza kiapo chake alichowaapia baba zenu, ndiyo sababu BWANA akawatoa kwa mkono wa nguvu, akawakomboa katika nyumba ya utumwa, katika mkono wa Farao, mfalme wa Misri.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini ni kwa sababu Mwenyezi-Mungu anawapenda na anashika kiapo alichowaapia babu zenu, ndiyo maana aliwaokoeni kwa mkono wake wenye nguvu na kuwaokoa toka utumwani, toka mikono ya Farao mfalme wa Misri.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
ila kwa kuwa Bwana aliwapenda ninyi, akataka kukitimiza kiapo, alichowaapia baba zenu, kwa hiyo Bwana aliwatoa ninyi kwa mkono wake wenye nguvu, akawakomboa mkononi mwa Farao, mfalme wa Misri, na kuwatoa nyumbani, mlimokuwa watumwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
bali kwa sababu BWANA anawapenda, na kwa sababu alitaka kuutimiza uapo wake aliowaapia baba zenu, ndiyo sababu BWANA akawatoa kwa mkono wa nguvu, akawakomboa katika nyumba ya utumwa, katika mkono wa Farao, mfalme wa Misri.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini ni kwa sababu Yawe anawapenda na anashika kiapo alichowaapia babu zenu, ndiyo maana aliwaokoa kwa nguvu zake kubwa na kuwaokoa toka katika utumwa, toka mikono ya mufalme wa Misri.