Deuteronomy 8:19 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini mkimsahau Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, na kuifuata miungu mingine ili kuitumikia na kuiabudu, nawaonyeni vikali leo hii kuwa hakika mtaangamia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ikiwa mtamsahau Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, mkaifuata miungu mingine, mkaiabudu na kuisujudia, ninashuhudia dhidi yenu leo kwamba hakika mtaangamizwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini itakuwa, kama ukimsahau Bwana, Mungu wako, na kuiandama miungu mingine, na kuitumikia na kuiabudu, nawashuhudia leo ya kuwa mtaangamia bila shaka.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini mkimsahau Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, na kuifuata miungu mingine ili kuitumikia na kuiabudu, nawaonyeni vikali leo hii kuwa hakika mtaangamia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ikiwa mtamsahau BWANA Mungu wenu, mkaifuata miungu mingine, mkaiabudu na kuisujudia, ninashuhudia dhidi yenu leo kwamba hakika mtaangamizwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ikiwa mtamsahau bwana Mwenyezi Mungu wenu, mkaifuata miungu mingine, mkaiabudu na kuisujudia, ninashuhudia dhidi yenu leo kwamba hakika mtaangamizwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini itakuwa, kama ukimsahau BWANA, Mungu wako, na kuiandama miungu mingine, na kuitumikia na kuiabudu, nawaonya leo ya kuwa mtaangamia bila shaka.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini mkimsahau Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, na kuifuata miungu mingine ili kuitumikia na kuiabudu, nawaonyeni vikali leo hii kuwa hakika mtaangamia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini itakapokuwa, umsahau Bwana Mungu wako na kufuata miungu mingine, uitumikie na kuitambikia, ninawashuhudia leo, ya kuwa mtaangamia kabisa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini itakuwa, kama ukimsahau BWANA, Mungu wako, na kuiandama miungu mingine, na kuitumikia na kuiabudu, nawashuhudia leo ya kuwa mtaangamia bila shaka.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini mukimusahau Yawe, Mungu wenu, na kufuata miungu mingine kwa kuitumikia na kuiabudu, ninawaonya vikali leo hii kwamba hakika mutaangamia.