Deuteronomy 8:9 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Huko mtapata chakula tele na hamtapungukiwa kitu. Miamba yake ina chuma, na kwenye milima yake mnaweza kuchimba shaba.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
nchi ambayo chakula hakitapungua na hamtakosa chochote; nchi ambayo miamba yake ni chuma na mnaweza kuchimba shaba kwenye vilima.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
nchi utakayokula mikate humo, pasina shida, hutapungukiwa na kitu ndani yake; nchi ambayo mawe yake ni chuma, na milima yake yafukuka shaba.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Huko mtapata chakula tele na hamtapungukiwa kitu. Miamba yake ina chuma, na kwenye milima yake mnaweza kuchimba shaba.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
nchi ambayo chakula hakitapungua na hamtakosa cho chote; nchi ambayo miamba yake ni chuma na mnaweza kuchimba shaba kutoka kwenye vilima.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
nchi ambayo chakula hakitapungua na hamtakosa chochote; nchi ambayo miamba yake ni chuma na mnaweza kuchimba shaba kutoka kwenye vilima.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
nchi utakayokula mikate humo, pasina shida, hutapungukiwa na kitu ndani yake; nchi ambayo mawe yake ni chuma, na milima yake mnaweza kuchimba shamba.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Huko mtapata chakula tele na hamtapungukiwa kitu. Miamba yake ina chuma, na kwenye milima yake mnaweza kuchimba shaba.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ni nchi, utakakokula chakula na kushiba sana, kwani hutakosa cho chote; ni nchi yenye mawe ya chuma, nazo shaba utazichimbua ndani ya milima yake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
nchi utakayokula mikate humo, pasina shida, hutapungukiwa na kitu ndani yake; nchi ambayo mawe yake ni chuma, na milima yake yafukuka shaba.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Huko mutapata chakula tele na hamutapungukiwa kitu. Mawe yake yana chuma, na kwenye milima yake munaweza kuchimba shaba.