Deuteronomy 9:16 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nilitazama, nikaona kwamba tayari mmekwisha kutenda dhambi dhidi ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu; mlikwisha jitengenezea sanamu ya ndama ya kusubu; bila kukawia mlikwisha iacha njia ya Mwenyezi-Mungu ambayo aliwaamuru.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nilipotazama, niliona kuwa mmefanya dhambi dhidi ya Mwenyezi Mungu, Mungu wenu; mmejifanyia sanamu ya kusubu katika umbo la ndama. Mmegeuka upesi kutoka njia ile Mwenyezi Mungu aliyowaagiza.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nikaangalia, na tazama, mlikuwa mmefanya dhambi juu ya Bwana, Mungu wenu; mmefanya ndama ya ng'ombe ya kusubu; mmekengeuka upesi katika njia aliyowaamuru Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nilitazama, nikaona kwamba tayari mmekwisha kutenda dhambi dhidi ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu; mlikwisha jitengenezea sanamu ya ndama ya kusubu; bila kukawia mlikwisha iacha njia ya Mwenyezi-Mungu ambayo aliwaamuru.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nilipotazama, niliona kuwa mmefanya dhambi dhidi ya BWANA Mungu wenu; mmejifanyia sanamu ya kusubu katika umbo la ndama. Mmegeuka upesi kutoka njia ile BWANA aliyowaagiza.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nilipotazama, niliona kuwa mmefanya dhambi dhidi ya bwana Mwenyezi Mungu wenu; mmejifanyia sanamu ya kusubu katika umbo la ndama. Mmegeuka upesi kutoka njia ile bwana aliyowaagiza.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nikaangalia, na tazama, mlikuwa mmefanya dhambi juu ya BWANA, Mungu wenu; mmefanya ndama ya ng'ombe ya kusubu; mmepotoka punde katika njia aliyowaamuru BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nilitazama, nikaona kwamba tayari mmekwisha kutenda dhambi dhidi ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu; mlikwisha jitengenezea sanamu ya ndama ya kusubu; bila kukawia mlikwisha iacha njia ya Mwenyezi-Mungu ambayo aliwaamuru.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nilipotazama niliona, ya kuwa mlimkosea Bwana Mungu wenu kwa kujifanyia kinyago cha ndama kilichoyeyushwa; ndivyo, mlivyoondoka upesi katika hiyo njia, Bwana aliyowaagiza.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nikaangalia, na tazama, mlikuwa mmefanya dhambi juu ya BWANA, Mungu wenu; mmefanya ndama ya ng’ombe ya kusubu; mmekengeuka upesi katika njia aliyowaamuru BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Niliangalia, nikaona kwamba mumekwisha kutenda zambi mbele ya Yawe, Mungu wenu. Mulikwisha kujitengenezea sanamu ya mwana-ngombe ya kuyeyushwa. Bila kukawia mulikwisha kuacha njia ya Yawe ambayo aliwaamuru.