Deuteronomy 9:18 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha nikalala chini kifudifudi mbele ya Mwenyezi-Mungu, kama hapo awali, kwa muda wa siku arubaini usiku na mchana; sikula chakula wala kunywa maji, kwa sababu ya dhambi mliyokuwa mmetenda kwa kufanya maovu mbele yake Mwenyezi-Mungu kwa kumkasirisha.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo tena nikasujudu hadi chini mbele za Mwenyezi Mungu kwa siku arobaini usiku na mchana. Sikula mkate wala sikunywa maji, kwa sababu ya dhambi yote mliyoifanya, mkifanya lile lililo ovu mbele za Mwenyezi Mungu na kumkasirisha.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nikaanguka nchi mbele za Bwana siku arobaini usiku na mchana, kama pale kwanza; sikula chakula wala kunywa maji; kwa sababu ya makosa yenu yote mliyokosa, kwa kufanya yaliyo maovu machoni pa Bwana, kwa kumkasirisha.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha nikalala chini kifudifudi mbele ya Mwenyezi-Mungu, kama hapo awali, kwa muda wa siku arubaini usiku na mchana; sikula chakula wala kunywa maji, kwa sababu ya dhambi mliyokuwa mmetenda kwa kufanya maovu mbele yake Mwenyezi-Mungu kwa kumkasirisha.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo tena nikasujudu mbele za BWANA kwa siku arobaini mchana na usiku. Sikula mkate wala sikunywa maji, kwa sababu ya dhambi yote mliyoifanya, mkifanya lile lililo ovu mbele za BWANA na kumkasirisha.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo tena nikasujudu mbele za bwana kwa siku arobaini usiku na mchana. Sikula mkate wala sikunywa maji, kwa sababu ya dhambi yote mliyoifanya, mkifanya lile lililo ovu mbele za bwana na kumkasirisha.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nikaanguka chini mbele za BWANA siku arobaini usiku na mchana, kama pale kwanza; sikula chakula wala kunywa maji; kwa sababu ya makosa yenu yote mliyofanya, kwa kufanya yaliyo maovu machoni pa BWANA, kwa kumkasirisha.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha nikalala chini kifudifudi mbele ya Mwenyezi-Mungu, kama hapo awali, kwa muda wa siku arubaini usiku na mchana; sikula chakula wala kunywa maji, kwa sababu ya dhambi mliyokuwa mmetenda kwa kufanya maovu mbele yake Mwenyezi-Mungu kwa kumkasirisha.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nikamwangukia Bwana kama ile mara ya kwanza siku 40 mchana kutwa na usiku kucha, sikula chakula, wala sikunywa maji kwa ajili ya makosa yenu yote, mliyoyakosa na kufanya yaliyokuwa mabaya machoni pake Bwana, yaliyomkasirisha.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nikaanguka nchi mbele za BWANA siku arobaini usiku na mchana, kama pale kwanza; sikula chakula wala kunywa maji; kwa sababu ya makosa yenu yote mliyokosa, kwa kufanya yaliyo maovu machoni pa BWANA, kwa kumkasirisha.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha nikalala uso mpaka chini mbele ya Yawe, kama vile mbele, kwa muda wa siku makumi ine usiku na muchana. Sikukula chakula wala kunywa maji, kwa sababu ya zambi muliyokuwa mumetenda kwa kufanya maovu mbele ya Yawe kwa kumukasirikisha.