Deuteronomy 9:25 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Kwa hiyo, nililala kifudifudi mbele ya Mwenyezi-Mungu siku hizo arubaini, usiku na mchana, kwa sababu Mwenyezi-Mungu alikuwa amesema atawaangamiza.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nilianguka kifudifudi mbele za Mwenyezi Mungu kwa zile siku arobaini usiku na mchana kwa sababu Mwenyezi Mungu alikuwa amesema angewaangamiza ninyi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo nikaanguka nchi mbele za Bwana siku zile arobaini usiku na mchana nilizokuwa nimeanguka nchi; kwa kuwa Bwana alisema atawaangamiza.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Kwa hiyo, nililala kifudifudi mbele ya Mwenyezi-Mungu siku hizo arubaini, usiku na mchana, kwa sababu Mwenyezi-Mungu alikuwa amesema atawaangamiza.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nilianguka kifudifudi mbele za BWANA kwa zile siku arobaini mchana na usiku kwa sababu BWANA alikuwa amesema angewaangamiza ninyi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nilianguka kifudifudi mbele za bwana kwa zile siku arobaini usiku na mchana kwa sababu bwana alikuwa amesema angewaangamiza ninyi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo nikaanguka chini mbele za BWANA siku zile arobaini usiku na mchana nilizokuwa nimeanguka chini; kwa kuwa BWANA alisema atawaangamiza.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Kwa hiyo, nililala kifudifudi mbele ya Mwenyezi-Mungu siku hizo arubaini, usiku na mchana, kwa sababu Mwenyezi-Mungu alikuwa amesema atawaangamiza.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hapo, nilipokuwa nimemwangukia Bwana hizo siku 40 mchana kutwa na usiku kucha, nilizolala chini, kwa kuwa Bwana alitaka kuwaangamiza ninyi,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo nikaanguka nchi mbele za BWANA siku zile arobaini usiku na mchana nilizokuwa nimeanguka nchi; kwa kuwa BWANA alisema atawaangamiza.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Kwa hiyo, nikalala uso mpaka chini mbele ya Yawe siku hizo makumi ine, usiku na muchana, kwa sababu Yawe alikuwa amesema atawaangamiza.