Deuteronomy 9:26 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nilimwomba Mwenyezi-Mungu, nikisema. ‘Ee Mwenyezi-Mungu, usiwaangamize watu wako na urithi wako, watu uliowakomboa na kuwatoa katika nchi ya Misri kwa uwezo na nguvu yako kubwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nilimwomba Mwenyezi Mungu na kusema, “Ee Bwana Mungu Mwenyezi, usiangamize watu wako, urithi wako mwenyewe ule ulioukomboa kwa uweza wako mkuu na kuwatoa katika nchi ya Misri kwa mkono wenye nguvu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nikamwomba Bwana, nikasema, Ee Bwana Mungu, usiwaangamize watu wako, urithi wako, uliowakomboa kwa ukuu wako, uliowatoa Misri kwa mkono wa nguvu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nilimwomba Mwenyezi-Mungu, nikisema. ‘Ee Mwenyezi-Mungu, usiwaangamize watu wako na urithi wako, watu uliowakomboa na kuwatoa katika nchi ya Misri kwa uwezo na nguvu yako kubwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nilimwomba BWANA na kusema, “Ee BWANA Mwenyezi, usiangamize watu wako, urithi wako mwenyewe ule ulioukomboa kwa uweza wako mkuu na kuwatoa katika nchi ya Misri kwa mkono wenye nguvu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nilimwomba bwana na kusema, “Ee bwana Mwenyezi, usiangamize watu wako, urithi wako mwenyewe ule ulioukomboa kwa uweza wako mkuu na kuwatoa katika nchi ya Misri kwa mkono wenye nguvu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nikamwomba BWANA, nikasema, Ee Bwana Mungu, usiwaangamize watu wako, urithi wako, uliowakomboa kwa ukuu wako, uliowatoa Misri kwa mkono wa nguvu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nilimwomba Mwenyezi-Mungu, nikisema. ‘Ee Mwenyezi-Mungu, usiwaangamize watu wako na urithi wako, watu uliowakomboa na kuwatoa katika nchi ya Misri kwa uwezo na nguvu yako kubwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
nikambembeleza Bwana kwamba: Bwana Mungu wangu, usiwaangamize walio ukoo wako, uliojipatia kuwa wako na kuwakomboa kwa ukuu wako ulipowatoa Misri kwa mkono wako wenye nguvu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nikamwomba BWANA, nikasema, Ee Bwana Mungu, usiwaangamize watu wako, urithi wako, uliowakomboa kwa ukuu wako, uliowatoa Misri kwa mkono wa nguvu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nikamwomba Yawe, nikisema: Ee Yawe, usiwaangamize watu wako na urizi wako, watu uliowakomboa na kuwatoa katika inchi ya Misri kwa uwezo na nguvu yako kubwa.