Deuteronomy 9:27 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakumbuke watumishi wako, Abrahamu, Isaka na Yakobo, wala usiujali ukaidi, uovu na dhambi za watu hawa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakumbuke watumishi wako Ibrahimu, Isaka na Yakobo. Usiangalie ukaidi wa watu hawa, uovu wao wala dhambi yao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakumbuke watumwa wako, Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo; usiangalie upotofu wa watu hawa, wala uovu wao, wala dhambi yao;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakumbuke watumishi wako, Abrahamu, Isaka na Yakobo, wala usiujali ukaidi, uovu na dhambi za watu hawa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakumbuke watumishi wako Abrahamu, Isaki na Yakobo. Usiangalie ukaidi wa watu hawa, uovu wao wala dhambi yao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakumbuke watumishi wako Ibrahimu, Isaka na Yakobo. Usiangalie ukaidi wa watu hawa, uovu wao wala dhambi yao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakumbuke watumishi wako, Abrahamu, na Isaka, na Yakobo; usiangalie ukaidi wa watu hawa, wala uovu wao, wala dhambi yao;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakumbuke watumishi wako, Abrahamu, Isaka na Yakobo, wala usiujali ukaidi, uovu na dhambi za watu hawa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakumbuke watumishi wako Aburahamu na Isaka na Yakobo, usiungalie ugumu wa watu hawa, wala uovu wao, wala ukosaji wao,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakumbuke watumwa wako, Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo; usiangalie upotofu wa watu hawa, wala uovu wao, wala dhambi yao;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Uwakumbuke watumishi wako, Abrahamu, Isaka na Yakobo, wala usijali ugumu, uovu na zambi za watu hawa.