Deuteronomy 9:28 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu wa kule ulikotutoa wasije wakasema, Mwenyezi-Mungu aliwatoa ili awaue jangwani kwa sababu hakuweza kuwaingiza katika nchi aliyowaahidi na kwa sababu aliwachukia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Watu wa nchi ile uliyotutoa sisi wasije wakasema, ‘Ni kwa sababu Mwenyezi Mungu hakuweza kuwachukua hadi nchi aliyokuwa amewaahidia, kwa sababu aliwachukia, akawaleta ili aje kuwaua jangwani.’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
isije nchi uliyotutoa ikasema, Ni kwa sababu Bwana hakuweza kuwaleta katika nchi aliyowapa ahadi, tena ni kwa kuwa aliwachukia, alivyowatoa nje ili kuwaua jangwani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu wa kule ulikotutoa wasije wakasema, Mwenyezi-Mungu aliwatoa ili awaue jangwani kwa sababu hakuweza kuwaingiza katika nchi aliyowaahidi na kwa sababu aliwachukia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Watu wa nchi ile uliyotutoa sisi wasije wakasema, ‘Ni kwa sababu BWANA hakuweza kuwachukua mpaka nchi aliyokuwa amewaahidia, kwa sababu aliwachukia, akawaleta ili aje kuwaua jangwani.’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Watu wa nchi ile uliyotutoa sisi wasije wakasema, ‘Ni kwa sababu bwana hakuweza kuwachukua mpaka nchi aliyokuwa amewaahidia, kwa sababu aliwachukia, akawaleta ili aje kuwaua jangwani.’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
isije nchi uliyotutoa ikasema, Ni kwa sababu BWANA hakuweza kuwaleta katika nchi aliyowahidi, tena ni kwa kuwa aliwachukia, aliwatoa nje ili kuwaua jangwani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu wa kule ulikotutoa wasije wakasema, Mwenyezi-Mungu aliwatoa ili awaue jangwani kwa sababu hakuweza kuwaingiza katika nchi aliyowaahidi na kwa sababu aliwachukia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
watu wa nchi hiyo, ulikotutoa, wasiseme: Bwana hakuweza kuwaingiza katika nchi ile, aliyowaagia, ila aliwatoa tu kwa kuwachukia, apate kuwaua nyikani.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
isije nchi uliyotutoa ikasema, Ni kwa sababu BWANA hakuweza kuwaleta katika nchi aliyowapa ahadi, tena ni kwa kuwa aliwachukia, alivyowatoa nje ili kuwaua jangwani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watu wa kule ulikotutoa wasiseme: ‘Yawe aliwatoa kusudi awaue katika jangwa kwa sababu hakuweza kuwaingiza katika inchi aliyowaahidi na kwa sababu aliwachukia’.