Deuteronomy 9:3 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Jueni leo hii kwamba anayewatangulia kama moto uteketezao miti ni Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu. Yeye atawaangamiza hao na kuwashinda mbele yenu; kwa hiyo mtawafukuza na kuwaangamiza mara moja, kama Mwenyezi-Mungu alivyowaahidi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kuweni na hakika leo kwamba Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, ndiye atakayetangulia kuvuka mbele yenu kama moto uteketezao. Atawaangamiza; atawatiisha mbele yenu. Nanyi mtawafukuza na kuwaangamiza mara moja, kama Mwenyezi Mungu alivyowaahidi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi jua siku hii ya leo kuwa Bwana, Mungu wako, ndiye atanguliaye kuvuka mbele yako kama moto uteketezao; atawaangamiza, tena atawaangusha mbele yako; ndivyo utakavyowafukuza na kuwapoteza upesi, kama alivyokuambia Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Jueni leo hii kwamba anayewatangulia kama moto uteketezao miti ni Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu. Yeye atawaangamiza hao na kuwashinda mbele yenu; kwa hiyo mtawafukuza na kuwaangamiza mara moja, kama Mwenyezi-Mungu alivyowaahidi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Iweni na hakika leo kwamba BWANA Mungu wenu ndiye atakayetangulia kuvuka mbele yenu kama moto uteketezao. Atawaangamiza; atawatiisha mbele yenu. Nanyi mtawafukuza na kuwaangamiza mara moja, kama BWANA alivyowaahidi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kuweni na hakika leo kwamba bwana Mwenyezi Mungu wenu ndiye atakayetangulia kuvuka mbele yenu kama moto uteketezao. Atawaangamiza; atawatiisha mbele yenu. Nanyi mtawafukuza na kuwaangamiza mara moja, kama bwana alivyowaahidi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi jua siku hii ya leo kuwa BWANA, Mungu wako, ndiye atanguliaye kuvuka mbele yako kama moto uteketezao; atawaangamiza, tena atawaangusha mbele yako; ndivyo utakavyowafukuza na kuwapoteza upesi, kama alivyokuambia BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Jueni leo hii kwamba anayewatangulia kama moto uteketezao miti ni Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu. Yeye atawaangamiza hao na kuwashinda mbele yenu; kwa hiyo mtawafukuza na kuwaangamiza mara moja, kama Mwenyezi-Mungu alivyowaahidi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo ujue leo hivi, ya kama Bwana Mungu wako ndiye atakayekutangulia kuvuka kuwa moto ulao, awaangamize na kuwaangusha chini mbele yako, upate kuwafukuza na kuwatowesha upesi, kama Bwana alivyokuambia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi jua siku hii ya leo kuwa BWANA, Mungu wako, ndiye atanguliaye kuvuka mbele yako kama moto uteketezao; atawaangamiza, tena atawaangusha mbele yako; ndivyo utakavyowafukuza na kuwapoteza upesi, kama alivyokuambia BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mujue leo hii kwamba anayewatangulia kama vile moto unaoteketeza miti ni Yawe, Mungu wenu. Atawaangamiza na kuwashinda mbele yenu, kwa hiyo mutawafukuza na kuwaangamiza mara moja, kama vile Yawe alivyowaahidi.