Deuteronomy 9:4 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Baada ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, kuwafukuza watu hao mbele yenu, msiseme moyoni mwenu kuwa, ‘Ni kwa sababu ya uadilifu wetu Mwenyezi-Mungu ametuleta tuimiliki nchi hii,’ ambapo Mwenyezi-Mungu amewafukuza watu hawa mbele yenu kwa sababu wao ni waovu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baada ya Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, kuwafukuza mbele yenu, msiseme mioyoni mwenu, “Mwenyezi Mungu ametuleta hapa kuimiliki nchi hii kwa sababu ya haki yetu.” La, ni kwa sababu ya uovu wa mataifa haya ndio Mwenyezi Mungu anawafukuza mbele yenu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Usiseme moyoni mwako, Bwana, Mungu wako, atakapokwisha kuwasukumia nje mbele yako, ukasema, Ni kwa haki yangu alivyonitia Bwana niimiliki nchi hii; kwani ni kwa ajili ya uovu wa mataifa haya Bwana awafukuza nje mbele yako.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Baada ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, kuwafukuza watu hao mbele yenu, msiseme moyoni mwenu kuwa, ‘Ni kwa sababu ya uadilifu wetu Mwenyezi-Mungu ametuleta tuimiliki nchi hii,’ ambapo Mwenyezi-Mungu amewafukuza watu hawa mbele yenu kwa sababu wao ni waovu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Baada ya BWANA Mungu wenu kuwafukuza mbele yenu, msiseme mioyoni mwenu, “BWANA ametuleta hapa kuimiliki nchi hii kwa sababu ya haki yetu.” La, ni kwa sababu ya uovu wa mataifa haya kwamba BWANA anawafukuza mbele yenu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Baada ya bwana Mwenyezi Mungu wenu kuwafukuza mbele yenu, msiseme mioyoni mwenu, “ bwana ametuleta hapa kuimiliki nchi hii kwa sababu ya haki yetu.” La, ni kwa sababu ya uovu wa mataifa haya ndiyo bwana anawafukuza mbele yenu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Usiseme moyoni mwako, BWANA, Mungu wako, atakapokwisha kuwasukumia nje mbele yako, ukasema, Ni kwa haki yangu alivyonitia BWANA niimiliki nchi hii; kwani ni kwa ajili ya uovu wa mataifa haya BWANA anawafukuza nje mbele yako.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Baada ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, kuwafukuza watu hao mbele yenu, msiseme moyoni mwenu kuwa, ‘Ni kwa sababu ya uadilifu wetu Mwenyezi-Mungu ametuleta tuimiliki nchi hii,’ ambapo Mwenyezi-Mungu amewafukuza watu hawa mbele yenu kwa sababu wao ni waovu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Bwana Mungu wako atakapowakimbiza mbele yako, usiseme moyoni mwako kwamba: Ni kwa ajili ya wongofu wetu, Bwana akituleta huku, tuichukue nchi hii, iwe yetu. Kwani ni kwa ajili ya uovu wao hao wamizimu, Bwana akiwafukuza mbele yako.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Usiseme moyoni mwako, BWANA, Mungu wako, atakapokwisha kuwasukumia nje mbele yako, ukasema, Ni kwa haki yangu alivyonitia BWANA niimiliki nchi hii; kwani ni kwa ajili ya uovu wa mataifa haya BWANA awafukuza nje mbele yako.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Yawe, Mungu wenu akiacha kuwafukuza watu hao mbele yenu, musiseme ndani ya moyo wenu kwamba: ‘Ni kwa sababu ya uhaki wetu Yawe ametuleta tuirizi inchi hii’, ambapo Yawe amewafukuza watu hawa mbele yenu kwa sababu wao ni waovu.