Deuteronomy 9:7 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Kumbukeni na msisahau jinsi mlivyomkasirisha Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, kule jangwani. Tangu siku ile mlipotoka nchi ya Misri mpaka siku mlipofika mahali hapa, nyinyi mmekuwa mkimwasi Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kumbukeni hili, kamwe msisahau jinsi mlivyomkasirisha Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, kwa hasira huko jangwani. Tangu siku mlipotoka Misri hadi mlipofika hapa, mmekuwa waasi dhidi ya Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kumbuka, usisahau ulivyomtia Bwana, Mungu wako, kasirani jangwani; tangu siku uliyotoka nchi ya Misri hata mlipofika mahali hapa, mmekuwa na uasi juu ya Bwana
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Kumbukeni na msisahau jinsi mlivyomkasirisha Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, kule jangwani. Tangu siku ile mlipotoka nchi ya Misri mpaka siku mlipofika mahali hapa, nyinyi mmekuwa mkimwasi Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kumbukeni hili, kamwe msisahau jinsi mlivyomkasirisha BWANA Mungu wenu kwa hasira huko jangwani. Tangu siku mlipotoka Misri mpaka mlipofika hapa, mmekuwa waasi dhidi ya BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kumbukeni hili, kamwe msisahau jinsi mlivyomkasirisha bwana Mwenyezi Mungu wenu kwa hasira huko jangwani. Tangu siku mlipotoka Misri mpaka mlipofika hapa, mmekuwa waasi dhidi ya bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kumbuka, usisahau ulivyomtia BWANA, Mungu wako, kasirani jangwani; tangu siku uliyotoka nchi ya Misri hadi mlipofika mahali hapa, mmekuwa na uasi juu ya BWANA
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Kumbukeni na msisahau jinsi mlivyomkasirisha Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, kule jangwani. Tangu siku ile mlipotoka nchi ya Misri mpaka siku mlipofika mahali hapa, nyinyi mmekuwa mkimwasi Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kumbuka, usisahau, ulivyomkasirisha Bwana Mungu wako nyikani! Tangu siku ile, ulipotoka katika nchi ya Misri, mpaka mlipofika mahali hapa, mlikuwa mkikataa kumtii Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kumbuka, usisahau ulivyomtia BWANA, Mungu wako, kasirani jangwani; tangu siku uliyotoka nchi ya Misri hata mlipofika mahali hapa, mmekuwa na uasi juu ya BWANA
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Mukumbuke na musisahau jinsi mulivyomukasirikisha Yawe, Mungu wenu, kule katika jangwa. Tangu siku ile mulipotoka katika inchi ya Misri mpaka siku mulipofika pahali hapa, ninyi mumekuwa mukimwasi Yawe.