Ecclesiastes 1:6 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Upepo wavuma kusini, wazunguka hadi kaskazini. Wavuma na kuvuma tena, warudia mzunguko wake daima.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Upepo huvuma kuelekea kusini na kugeukia kaskazini; hurudia mzunguko huo huo, daima ukirudia njia yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Upepo huvuma kusi, hugeuka kuwa kaskazi; hugeuka daima katika mwendo wake, na upepo huyarudia mazunguko yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Upepo wavuma kusini, wazunguka hadi kaskazini. Wavuma na kuvuma tena, warudia mzunguko wake daima.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Upepo huvuma kuelekea kusini na kugeukia kaskazini, hurudia mzunguko huo huo, daima ukirudia njia yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Upepo huvuma kuelekea kusini na kugeukia kaskazini, hurudia mzunguko huo huo, daima ukirudia njia yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Upepo huvuma kuelekea kusini, kisha huvuma kuelekea kaskazini; hugeuka daima katika mwendo wake, nao huyarudia mazunguko yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Upepo wavuma kusini, wazunguka hadi kaskazini. Wavuma na kuvuma tena, warudia mzunguko wake daima.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Upepo ukienda kusini, kisha hugeuka kwenda kaskazini; ndivyo, upepo unavyojiendea na kugeukageuka. Kwa kugeukageuka kwake upepo hurudia hapo, ulipotokea.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Upepo huvuma kusi, hugeuka kuwa kaskazi; hugeuka daima katika mwendo wake, na upepo huyarudia mazunguko yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Upepo unavuma tokea kusini, unazunguka mpaka kaskazini. Unazungukazunguka katika mwendo wake, kisha unarudia tena katika muzunguko wake siku zote.