Ecclesiastes 10:1 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nzi waliokufa husababisha marashi kunuka; upumbavu kidogo hubatilisha hekima na heshima.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kama vile inzi waliokufa huacha harufu mbaya kwenye manukato, ndivyo upumbavu kidogo huzidi nguvu hekima na heshima.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mainzi mafu huvundisha marhamu ya mwuza marashi; Kadhalika upumbavu haba ni mzito kuliko hekima na heshima.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nzi waliokufa husababisha marashi kunuka; upumbavu kidogo hubatilisha hekima na heshima.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kama vile mainzi waliokufa huacha harufu mbaya kwenye manukato, ndivyo upumbavu kidogo huzidi nguvu hekima na heshima.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kama vile nzi waliokufa huacha harufu mbaya kwenye manukato, ndivyo upumbavu kidogo huzidi nguvu hekima na heshima.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nzi waliokufa hufanya manukato ya mwuza marashi kutoa uvundo; Kadhalika upumbavu haba ni mzito kuliko hekima na heshima.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nzi waliokufa husababisha marashi kunuka; upumbavu kidogo hubatilisha hekima na heshima.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mainzi waliokufa huyaozesha kwa kuyachafua mafuta ya mtengeneza manukato, ujinga hufanya makuu kuliko werevu wa kweli na utukufu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mainzi mafu huvundisha marhamu ya mwuza marashi; Kadhalika upumbavu haba ni mzito kuliko hekima na heshima.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mainzi waliokufa wanaharibu na kunukisha marasi; upumbafu kidogo unapoteza hekima na heshima.