Ecclesiastes 11:9 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ewe kijana, furahia ujana wako, moyo wako, uchangamke wakati ungali kijana. Fuata mapenzi ya moyo wako na upeo wa macho yako. Lakini kumbuka kwamba Mungu atakuhukumu kadiri ya hayo yote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Furahi ewe kijana, ukiwa bado kijana, moyo wako na ukupe furaha siku za ujana wako. Fuata njia za moyo wako na chochote macho yako yanaona, lakini ujue kwamba kwa ajili ya haya yote Mungu atakuleta hukumuni.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wewe kijana, uufurahie ujana wako, na moyo wako ukuchangamshe siku za ujana wako, ukaziendee njia za moyo wako, na katika maono ya macho yako, lakini ujue wewe ya kwamba kwa ajili ya hayo yote Mungu atakuleta hukumuni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ewe kijana, furahia ujana wako, moyo wako, uchangamke wakati ungali kijana. Fuata mapenzi ya moyo wako na upeo wa macho yako. Lakini kumbuka kwamba Mungu atakuhukumu kadiri ya hayo yote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Furahi ewe kijana, wakati ungali kijana, moyo wako na ukupe furaha katika siku za ujana wako. Fuata njia za moyo wako na cho chote macho yako yaonayo, lakini ujue kwamba kwa ajili ya haya yote Mungu atakuleta hukumuni.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Furahi ewe kijana, wakati ungali kijana, moyo wako na ukupe furaha katika siku za ujana wako. Fuata njia za moyo wako na chochote macho yako yaonayo, lakini ujue kwamba kwa ajili ya haya yote Mungu atakuleta hukumuni.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wewe kijana, uufurahie ujana wako, na moyo wako ukuchangamshe siku za ujana wako, ukaziendee njia za moyo wako, na kinachotamaniwa na macho yako, lakini ujue wewe ya kwamba kwa ajili ya hayo yote Mungu atakuleta hukumuni.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ewe kijana, furahia ujana wako, moyo wako, uchangamke wakati ungali kijana. Fuata mapenzi ya moyo wako na upeo wa macho yako. Lakini kumbuka kwamba Mungu atakuhukumu kadiri ya hayo yote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wewe kijana, ufurahie utoto wako, moyo wako ule mema siku za ujana wako! Kazishike njia, moyo wako uzitakazo, kayafuate, macho yako yanayoyatazamia! Lakini ujue, ya kuwa hayo yote Mungu atakutakia shauri.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wewe kijana, uufurahie ujana wako, na moyo wako ukuchangamshe siku za ujana wako, ukaziendee njia za moyo wako, na katika maono ya macho yako, lakini ujue wewe ya kwamba kwa ajili ya hayo yote Mungu atakuleta hukumuni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ewe kijana, furahia ujana wako, moyo wako ukuwe na raha wakati ungali kijana. Fuata mapenzi ya moyo wako na tamaa ya macho yako. Lakini kumbuka kwamba Mungu atakuhukumu kadiri ya hayo yote.