Ecclesiastes 2:10 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kila macho yangu yalichokitamani nilikipata. Moyo wangu sikuunyima raha yoyote ile; kwa kuwa moyo wangu ulifurahia niliyotenda, na hili lilikuwa tuzo la jasho langu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Sikujinyima kitu chochote ambacho macho yangu yalikitamani, hakuna anasa niliyounyima moyo wangu. Moyo wangu ulifurahia kazi zangu zote, hii ilikuwa thawabu ya kazi zangu zote.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wala sikuyanyima macho yangu cho chote yalichokitamani; wala sikuuzuia moyo wangu katika furaha yo yote; maana moyo wangu ulifurahi kwa sababu ya kazi yangu yote, na hii ilikuwa sehemu yangu katika kazi yangu yote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kila macho yangu yalichokitamani nilikipata. Moyo wangu sikuunyima raha yoyote ile; kwa kuwa moyo wangu ulifurahia niliyotenda, na hili lilikuwa tuzo la jasho langu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Sikujinyima kitu cho chote ambacho macho yangu yalikitamani, hakuna anasa ambayo niliunyima moyo wangu. Moyo wangu ulifurahia kazi zangu zote, hii ilikuwa thawabu ya kazi zangu zote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Sikujinyima kitu chochote ambacho macho yangu yalikitamani, hakuna anasa ambayo niliunyima moyo wangu. Moyo wangu ulifurahia kazi zangu zote, hii ilikuwa thawabu ya kazi zangu zote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wala sikuyanyima macho yangu chochote yalichokitamani; wala sikuuzuia moyo wangu katika furaha yoyote; maana moyo wangu ulifurahi kwa sababu ya kazi yangu yote, na hii ilikuwa sehemu yangu katika kazi yangu yote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kila macho yangu yalichokitamani nilikipata. Moyo wangu sikuunyima raha yoyote ile; kwa kuwa moyo wangu ulifurahia niliyotenda, na hili lilikuwa tuzo la jasho langu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yote, macho yangu yaliyoyatamani, hakuna nilichoyanyima; wala moyo wangu sikuukataza furaha yo yote. Kwani moyo wangu uliyafurahia yote, niliyoyasumbukia, tena furaha hii ilikuwa pato langu, nililojipatia kwa masumbuko yangu yote.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wala sikuyanyima macho yangu cho chote yalichokitamani; wala sikuuzuia moyo wangu katika furaha yo yote; maana moyo wangu ulifurahi kwa sababu ya kazi yangu yote, na hii ilikuwa sehemu yangu katika kazi yangu yote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kila kitu macho yangu yalichokitamani nilikipata. Moyo wangu sikuunyima raha yoyote. Moyo wangu ulifurahia mambo niliyotenda, na hii ilikuwa zawadi ya jasho langu.