Ecclesiastes 2:3 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nilifikiria sana, namna ya kujichangamsha akili kwa divai, huku nikisukumwa na ari yangu ya kupata hekima; pia namna ya kuandamana na upumbavu ili nione yaliyo bora kabisa ambayo wanadamu wanaweza wakafanya waishipo maisha yao mafupi hapa duniani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nikajaribu kujifurahisha kwa mvinyo na kukumbatia upumbavu, huku bado akili yangu inaniongoza kwa hekima. Nilitaka kuona ni lipi bora watu wafanye kwa siku chache wanazoishi chini ya mbingu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Moyoni mwangu nikapeleleza jinsi ya kuuburudisha mwili kwa mvinyo, na (moyo wangu ukali ukiniongoza kwa hekima) jinsi ya kushikana na upumbavu, hata niyaone yaliyo mema ya kuwafaa wanadamu, ili wayafanye hayo chini ya mbingu siku zote za maisha yao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nilifikiria sana, namna ya kujichangamsha akili kwa divai, huku nikisukumwa na ari yangu ya kupata hekima; pia namna ya kuandamana na upumbavu ili nione yaliyo bora kabisa ambayo wanadamu wanaweza wakafanya waishipo maisha yao mafupi hapa duniani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nikajaribu kujifurahisha kwa mvinyo na kukumbatia upumbavu, huku bado akili yangu inaniongoza kwa hekima. Nilitaka kuona ni lipi bora watu wafanye kwa siku chache wanazoishi chini ya mbingu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nikajaribu kujifurahisha kwa mvinyo na kukumbatia upumbavu, huku bado akili yangu inaniongoza kwa hekima. Nilitaka kuona ni lipi bora watu wafanye kwa siku chache wanazoishi chini ya mbingu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Moyoni mwangu nikapeleleza jinsi ya kuuburudisha mwili kwa mvinyo, na (moyo wangu ungali ukiniongoza kwa hekima) jinsi ya kushikana na upumbavu, hata niyaone yaliyo mema ya kuwafaa wanadamu, ili wayafanye hayo chini ya mbingu siku zote za maisha yao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nilifikiria sana, namna ya kujichangamsha akili kwa divai, huku nikisukumwa na ari yangu ya kupata hekima; pia namna ya kuandamana na upumbavu ili nione yaliyo bora kabisa ambayo wanadamu wanaweza wakafanya waishipo maisha yao mafupi hapa duniani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Niliwaza moyoni mwangu kuufurahisha mwili wangu kwa mvinyo, lakini akili zikae zikiuongoza mwili; nikataka kuufuata huo ujinga, mpaka niyaone yawafaliayo wana wa Adamu kuyafanya chini ya mbingu siku zao zote za kuwapo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Moyoni mwangu nikapeleleza jinsi ya kuuburudisha mwili kwa mvinyo, na (moyo wangu ukali ukiniongoza kwa hekima) jinsi ya kushikana na upumbavu, hata niyaone yaliyo mema ya kuwafaa wanadamu, ili wayafanye hayo chini ya mbingu siku zote za maisha yao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nilitafuta kwa hekima namna ya kujichangamusha mwili kwa divai na kutenda sawa na wapumbafu. Nilitaka kuona kitu gani ni kizuri kwa wanadamu kufanya wanapoishi maisha yao mafupi hapa chini ya mbingu.