Ecclesiastes 4:1 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha nikaona udhalimu wote unaofanyika duniani. Watu wanaokandamizwa hulia machozi, lakini hakuna yeyote anayewafariji. Wakandamizaji wao wana nguvu, ndiyo sababu hakuna wa kuwafariji.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nikatazama tena nikaona uonevu wote uliokuwa unafanyika chini ya jua: Nikaona machozi ya waliodhulumiwa, wala hawana mfariji; uwezo ulikuwa upande wa wale wanaowadhulumu, lakini hawakuwa na mfariji.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha nikarudi na kuona madhalimu yote yanayotendeka chini ya jua; na tazama, machozi yao waliodhulumiwa, ambao walikuwa hawana mfariji; na upande wa wale waliowadhulumu kulikuwa na uwezo, walakini wale walikuwa hawana mfariji.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha nikaona udhalimu wote unaofanyika duniani. Watu wanaokandamizwa hulia machozi, lakini hakuna yeyote anayewafariji. Wakandamizaji wao wana nguvu, ndiyo sababu hakuna wa kuwafariji.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nikatazama tena nikaona uonevu wote uliokuwa unafanyika chini ya jua: Nikaona machozi ya walioonewa, wala hawana wa kuwafariji; uwezo ulikuwa upande wa wale wanaowaonea, wala hawana wa kuwafariji.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nikatazama tena nikaona uonevu wote uliokuwa unafanyika chini ya jua: Nikaona machozi ya walioonewa, wala hawana wa kuwafariji; uwezo ulikuwa upande wa wale wanaowaonea, wala hawana wa kuwafariji.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha nikarudi na kuona udhalimu wote unaotendeka chini ya jua; na tazama, machozi yao waliodhulumiwa, ambao walikuwa hawana mfariji; na upande wa wale waliowadhulumu kulikuwa na uwezo, lakini wale walikuwa hawana mfariji.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha nikaona udhalimu wote unaofanyika duniani. Watu wanaokandamizwa hulia machozi, lakini hakuna yeyote anayewafariji. Wakandamizaji wao wana nguvu, ndiyo sababu hakuna wa kuwafariji.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nilipoyatazama tena makorofi yanayofanywa chini ya jua, niliona machozi yao waliokorofishwa, lakini sikuona aliyewatuliza mioyo; namo mikononi mwao waliowakorofisha zimo nguvu, kwa hiyo kwao hakuna atakayewatuliza mioyo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha nikarudi na kuona madhalimu yote yanayotendeka chini ya jua; na tazama, machozi yao waliodhulumiwa, ambao walikuwa hawana mfariji; na upande wa wale waliowadhulumu kulikuwa na uwezo, walakini wale walikuwa hawana mfariji.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha nikaona mateso yote yanayofanyika chini ya jua. Watu wanaogandamizwa wanalia machozi, lakini hakuna mutu yeyote anayewafariji. Wagandamizaji wao wana nguvu, ndiyo sababu hakuna wa kuwafariji.