Ecclesiastes 5:19 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kama Mungu anampa mtu utajiri na mali na kumjalia fursa ya kufurahia hayo, basi binadamu ashukuru na avifaidi hivyo alivyojipatia kwa jasho lake. Hiyo ni zawadi kutoka kwa Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Zaidi ya yote, Mungu anapompa mtu yeyote utajiri na milki, humwezesha kuvifurahia, kukubali fungu lake na kuwa na furaha katika kazi yake, hii ni karama ya Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena, kwa habari za kila mwanadamu, ambaye Mungu amempa mali na ukwasi, akamwezesha kula katika hizo, na kuipokea sehemu yake, na kuifurahia amali yake; hiyo ndiyo karama ya Mungu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kama Mungu anampa mtu utajiri na mali na kumjalia fursa ya kufurahia hayo, basi binadamu ashukuru na avifaidi hivyo alivyojipatia kwa jasho lake. Hiyo ni zawadi kutoka kwa Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Zaidi ya yote, Mungu anapompa mtu ye yote utajiri na milki, humwezesha kuvifurahia, kukubali fungu lake na kuwa na furaha katika kazi yake, hii ni karama ya Mungu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Zaidi ya yote, Mungu anapompa mtu yeyote utajiri na milki, humwezesha kuvifurahia, kukubali fungu lake na kuwa na furaha katika kazi yake, hii ni karama ya Mungu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena, kwa habari za kila mwanadamu, ambaye Mungu amempa mali na ukwasi, akamwezesha kula katika hizo, na kuipokea sehemu yake, na kuifurahia amali yake; hiyo ndiyo karama ya Mungu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kama Mungu anampa mtu utajiri na mali na kumjalia fursa ya kufurahia hayo, basi binadamu ashukuru na avifaidi hivyo alivyojipatia kwa jasho lake. Hiyo ni zawadi kutoka kwa Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tena mtu ye yote, Mungu aliyemgawia mali na mema ya dunia hii na kumpa uwezo wa kuyala na kulichukua fungu lake na kuyafurahia masumbuko yake, basi, ajue, ya kuwa hilo ndilo gawio lake Mungu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena, kwa habari za kila mwanadamu, ambaye Mungu amempa mali na ukwasi, akamwezesha kula katika hizo, na kuipokea sehemu yake, na kuifurahia amali yake; hiyo ndiyo karama ya Mungu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na kwa kuwa Mungu amemuruhusu kuwa na furaha, mwanadamu hatakuwa na wasiwasi mwingi juu ya maisha yake mafupi.