Ecclesiastes 5:8 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Usishangae ukiona katika nchi watu fukara wanakandamizwa, wananyimwa haki zao na maslahi yao. Kila mwenye cheo anayewadhulumu wanyonge yupo chini ya mkuu mwingine, na juu ya hao wote kuna wakuu zaidi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ukiona maskini wanaodhulumiwa katika nchi, na hukumu na haki vikipotoshwa, usishangazwe na mambo hayo; kwa maana afisa mmoja anaangaliwa na aliye juu yake, na juu ya hao wawili kuna wengine walio juu yao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ujapokuwa unaona maskini kuonewa, na hukumu na haki kuondolewa kwa jeuri katika jimbo, usilistaajabie jambo hilo; kwa sababu, Aliye juu kuliko walio juu huangalia; Tena wako walio juu kupita hao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Usishangae ukiona katika nchi watu fukara wanakandamizwa, wananyimwa haki zao na maslahi yao. Kila mwenye cheo anayewadhulumu wanyonge yupo chini ya mkuu mwingine, na juu ya hao wote kuna wakuu zaidi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kama ukiona maskini wanaonewa katika nchi, hukumu na haki vikipotoshwa, usishangazwe na mambo hayo, kwa maana afisa mmoja anaangaliwa na aliye juu yake zaidi na juu ya hao wawili kuna wengine walio juu zaidi yao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kama ukiona maskini wanaonewa katika nchi, hukumu na haki vikipotoshwa, usishangazwe na mambo hayo, kwa maana afisa mmoja anaangaliwa na aliye juu yake zaidi na juu ya hao wawili kuna wengine walio juu zaidi yao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ujapokuwa unaona maskini kuonewa, na hukumu na haki kuondolewa kwa jeuri katika jimbo, usilistaajabie jambo hilo; kwa sababu, Aliye Juu kuliko walio juu huangalia; Tena wako walio juu kupita hao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Usishangae ukiona katika nchi watu fukara wanakandamizwa, wananyimwa haki zao na maslahi yao. Kila mwenye cheo anayewadhulumu wanyonge yupo chini ya mkuu mwingine, na juu ya hao wote kuna wakuu zaidi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ukiona, maskini akikorofishwa, tena mashauri yaliyo sawa nayo mambo yaongokayo yakiondolewa mjini kwa nguvu, usivistaajabu, vikifanyika hivyo! Kwani aliye mkuu yuko na mkuu kumpita amwangaliaye, tena juu yao wote yuko aliye mkuu mwenyewe.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ujapokuwa unaona maskini kuonewa, na hukumu na haki kuondolewa kwa jeuri katika jimbo, usilistaajabie jambo hilo; kwa sababu, Aliye juu kuliko walio juu huangalia; Tena wako walio juu kupita hao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Faida ya mavuno ya inchi ni kwa watu wote, hata mufalme vilevile anatumainia mavuno yale.