Ecclesiastes 8:17 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
halafu niliona kazi yote ya Mungu ya kwamba mwanadamu hawezi kuelewa kazi inayofanyika duniani. Wenye hekima wanaweza kujidai eti wanajua, lakini, kwa kweli, hawajui.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
ndipo nikaona yale yote ambayo Mungu ameyafanya. Hakuna yeyote awezaye kuelewa yale yanayotendeka chini ya jua. Licha ya juhudi zake zote za kutafuta, mtu hawezi kugundua maana yake. Hata ingawa mtu mwenye hekima anadai kuwa anafahamu, kwa hakika hawezi kutambua.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
basi, niliiona kazi yote ya Mungu, ya kuwa haitafutikani na mwanadamu kazi inayofanyika chini ya jua; kwa sababu mwanadamu na akijisumbua kadiri awezavyo kuitafuta, hata hivyo hataiona; naam, zaidi ya hayo, mwenye hekima ajapodhania ya kuwa ataijua, lakini yeye hataweza kuiona.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
halafu niliona kazi yote ya Mungu ya kwamba mwanadamu hawezi kuelewa kazi inayofanyika duniani. Wenye hekima wanaweza kujidai eti wanajua, lakini, kwa kweli, hawajui.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
ndipo nikaona yale yote ambayo Mungu ameyafanya. Hakuna ye yote awezaye kuelewa yale yanayotendeka chini ya jua. Licha ya juhudi zake zote za kutafuta, mtu hawezi kugundua maana yake. Hata ingawa mtu mwenye hekima anadai kuwa anafahamu, kwa hakika hawezi kutambua.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
ndipo nikaona yale yote ambayo Mungu ameyafanya. Hakuna yeyote awezaye kuelewa yale yanayotendeka chini ya jua. Licha ya juhudi zake zote za kutafuta, mtu hawezi kugundua maana yake. Hata ingawa mtu mwenye hekima anadai kuwa anafahamu, kwa hakika hawezi kutambua.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
basi, niliiona kazi yote ya Mungu, ya kuwa haifahamiki na mwanadamu kazi inayofanyika chini ya jua; kwa sababu hata mwanadamu akijisumbua kadiri awezavyo kuichunguza, hataiona; naam, zaidi ya hayo, hata ingawa mwenye hekima hadai anajua, wao hawawezi kuifahamu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
halafu niliona kazi yote ya Mungu ya kwamba mwanadamu hawezi kuelewa kazi inayofanyika duniani. Wenye hekima wanaweza kujidai eti wanajua, lakini, kwa kweli, hawajui.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, nilipozitazama kazi zote za Mungu, nikaona, ya kuwa mtu hawezi kuzitambua maana hizo kazi zinazofanywa chini ya jua; ijapo mtu ajisumbue sana kwa kuitafuta hiyo maana, haioni. Hata mwerevu wa kweli akijiwazia kwamba ameijua, hawezi kuitambua.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
basi, niliiona kazi yote ya Mungu, ya kuwa haitafutikani na mwanadamu kazi inayofanyika chini ya jua; kwa sababu mwanadamu na akijisumbua kadiri awezavyo kuitafuta, hata hivyo hataiona; naam, zaidi ya hayo, mwenye hekima ajapodhania ya kuwa ataijua, lakini yeye hataweza kuiona.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
lakini hataelewa kazi ya Mungu inayofanyika chini ya jua. Mutu anaweza kutoa jasho sana lakini hataelewa. Wenye hekima wanaweza kujidai kwamba wanajua, lakini, kwa kweli, hawajui.