Ecclesiastes 8:9 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Haya yote nimeyaona katika uchunguzi wangu juu ya yote yanayotendwa hapa duniani, binadamu anapokuwa na uwezo wa kumkandamiza na kumdhuru binadamu mwenzake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yote haya niliyaona, nilipokuwa natafakari kila kitu kinachotendeka chini ya jua. Kuna wakati mtu hujifanya bwana juu ya wengine kwa madhara yake mwenyewe.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mambo hayo yote nimeyaona, nikatia moyo wangu katika kila kazi iliyofanyika chini ya jua. Kuna wakati ambapo mtu mmoja anayo mamlaka juu ya mwenziwe kwa hasira yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Haya yote nimeyaona katika uchunguzi wangu juu ya yote yanayotendwa hapa duniani, binadamu anapokuwa na uwezo wa kumkandamiza na kumdhuru binadamu mwenzake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yote haya niliyaona, nilipokuwa natafakari kila kitu kinachotendeka chini ya jua. Kuna wakati ambapo mtu hujifanya bwana juu ya wengine kwa madhara yake mwenyewe.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yote haya niliyaona, nilipokuwa natafakari kila kitu kinachotendeka chini ya jua. Kuna wakati ambapo mtu hujifanya bwana juu ya wengine kwa madhara yake mwenyewe.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mambo hayo yote nimeyaona, nikatia moyo wangu katika kila kazi iliyofanyika chini ya jua. Kuna wakati ambapo mtu mmoja anayo mamlaka juu ya mwenziwe kwa hasira yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Haya yote nimeyaona katika uchunguzi wangu juu ya yote yanayotendwa hapa duniani, binadamu anapokuwa na uwezo wa kumkandamiza na kumdhuru binadamu mwenzake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hayo yote niliyatazama, nikayaweka moyoni mwangu, nikaziangalia kazi zote zinazofanywa chini ya jua, mtu anapomtawala mtu mwenziwe, apate kumfanyizia mabaya.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mambo hayo yote nimeyaona, nikatia moyo wangu katika kila kazi iliyofanyika chini ya jua. Kuna wakati ambapo mtu mmoja anayo mamlaka juu ya mwenziwe kwa hasira yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Haya yote nimeyaona katika uchunguzi wangu juu ya yote yanayotendeka hapa chini ya jua, ambako mwanadamu anatawala mwenzake na kumutesa.