Ecclesiastes 9:1 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nilitafakari juu ya hayo yote, nikaona kwamba Mungu anaongoza matendo ya watu wenye hekima na waadilifu; ikiwa ni upendo au chuki, binadamu hajui. Kila kitu kwao ni bure kabisa,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo niliyatafakari haya yote, nikafikia uamuzi kwamba waadilifu na wenye hekima na yale wanayoyafanya yako mikononi mwa Mungu, lakini hakuna mtu ajuaye kama anangojewa na upendo au chuki.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na kwa ajili ya hayo yote, nikatia moyo wangu katika kuyatafuta-tafuta haya; ya kuwa wenye haki, na wenye hekima, pamoja na matendo yao yote, wamo mkononi mwa Mungu; kwamba ni pendo au kwamba ni chuki, mwanadamu hajui; mambo yote yawapita.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nilitafakari juu ya hayo yote, nikaona kwamba Mungu anaongoza matendo ya watu wenye hekima na waadilifu; ikiwa ni upendo au chuki, binadamu hajui. Kila kitu kwao ni bure kabisa,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo niliyatafakari yote haya nikafikia uamuzi kwamba waadilifu na wenye hekima na yale wanayoyafanya yako mikononi mwa Mungu, lakini hakuna mtu ajuaye kama anangojewa na upendo au chuki.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo niliyatafakari yote haya nikafikia uamuzi kwamba waadilifu na wenye hekima na yale wanayoyafanya yako mikononi mwa Mungu, lakini hakuna mtu ajuaye kama anangojewa na upendo au chuki.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na kwa ajili ya hayo yote, nikatia moyo wangu katika kuyachunguza haya; ya kuwa wenye haki, na wenye hekima, pamoja na matendo yao yote, wamo mkononi mwa Mungu; iwe ni upendo au iwe ni chuki, mwanadamu hajui; mambo yote yawapita.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nilitafakari juu ya hayo yote, nikaona kwamba Mungu anaongoza matendo ya watu wenye hekima na waadilifu; ikiwa ni upendo au chuki, binadamu hajui. Kila kitu kwao ni bure kabisa,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hayo yote nikayaweka moyoni mwangu na kuyachunguza haya yote, ya kuwa waongofu na werevu wa kweli pamoja na kazi zao zote wamo mkononi mwa Mungu. Hakuna mtu ajuaye, kama ni kupenda au kama ni kuchukia kumpasako, yote pia yako yamefichika bado mbele yake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na kwa ajili ya hayo yote, nikatia moyo wangu katika kuyatafuta-tafuta haya; ya kuwa wenye haki, na wenye hekima, pamoja na matendo yao yote, wamo mkononi mwa Mungu; kwamba ni pendo au kwamba ni chuki, mwanadamu hajui; mambo yote yawapita.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nilifikiri sana juu ya hayo yote, nikaona kwamba Mungu anaongoza matendo ya watu wenye hekima na wenye haki; ikiwa ni upendo au chuki, mwanadamu hajui. Kila kitu kwao ni bure,