Ecclesiastes 9:11 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Tena, nimeona kitu kimoja hapa duniani, kwamba wenye mbio hawafaulu katika riadha, wala wenye nguvu hawashindi vita; wenye busara hawapati chakula, wenye akili hawatajiriki, wala wenye ujuzi hawapandi vyeo; lakini wakati wa bahati huwapata wote pamoja.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nimeona kitu kingine tena chini ya jua: Si wenye mbio washindao mashindano au wenye nguvu washindao vita, wala si wenye hekima wapatao chakula au wenye akili nyingi wapatao mali, wala wenye elimu wapatao upendeleo, lakini fursa huwapata wote.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nikarudi, na kuona chini ya jua, ya kwamba si wenye mbio washindao katika michezo, wala si walio hodari washindao vitani, wala si wenye hekima wapatao chakula, wala si watu wa ufahamu wapatao mali, wala wenye ustadi wapatao upendeleo; lakini wakati na bahati huwapata wote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Tena, nimeona kitu kimoja hapa duniani, kwamba wenye mbio hawafaulu katika riadha, wala wenye nguvu hawashindi vita; wenye busara hawapati chakula, wenye akili hawatajiriki, wala wenye ujuzi hawapandi vyeo; lakini wakati wa bahati huwapata wote pamoja.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nimeona kitu kingine tena chini ya jua: Si wenye mbio washindao mashindano au wenye nguvu washindao vita, wala si wenye hekima wapatao chakula au wenye akili nyingi wapatao mali, wala wenye elimu wapatao upendeleo, lakini fursa huwapata wote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nimeona kitu kingine tena chini ya jua: Si wenye mbio washindao mashindano au wenye nguvu washindao vita, wala si wenye hekima wapatao chakula au wenye akili nyingi wapatao mali, wala wenye elimu wapatao upendeleo, lakini fursa huwapata wote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nikarudi, na kuona chini ya jua, ya kwamba si wenye mbio washindao katika michezo, wala si walio hodari washindao vitani, wala si wenye hekima wapatao chakula, wala si watu wa ufahamu wapatao mali, wala wenye ustadi wapatao upendeleo; lakini wakati na bahati huwapata wote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Tena, nimeona kitu kimoja hapa duniani, kwamba wenye mbio hawafaulu katika riadha, wala wenye nguvu hawashindi vita; wenye busara hawapati chakula, wenye akili hawatajiriki, wala wenye ujuzi hawapandi vyeo; lakini wakati wa bahati huwapata wote pamoja.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nilipoyatazama tena yaliyoko chini ya jua, nikaona, ya kuwa sio wepesi washindao katika mashindano ya mbio, wala sio mafundi wa vita washindao vitani, wala sio werevu wa kweli wapatao vilaji, wala sio watambuzi wapatao mali, wala sio wajuzi wapendezao, kwani wao wote kila mmoja wao huwa na siku zake na mambo yake yatakayompata.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nikarudi, na kuona chini ya jua, ya kwamba si wenye mbio washindao katika michezo, wala si walio hodari washindao vitani, wala si wenye hekima wapatao chakula, wala si watu wa ufahamu wapatao mali, wala wenye ustadi wapatao upendeleo; lakini wakati na bahati huwapata wote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Tena, nimeona kitu kimoja hapa chini ya jua, kwamba wenye kukimbia mbio hawashindi katika mashindano ya kukimbia, wala wenye nguvu hawashindi vita, wenye hekima hawapati chakula, wenye akili hawatajiriki, wala wenye ujuzi hawapandi vyeo. Lakini wakati wa bahati unawapata wote pamoja.