Ecclesiastes 9:15 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Katika mji huo, alikuwapo maskini mmoja mwenye hekima, ambaye, kwa hekima yake aliuokoa mji huo. Lakini hakuna mtu aliyemkumbuka huyo maskini baadaye.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Katika mji huo kulikuwa na mtu mmoja maskini lakini mwenye hekima, naye akauokoa ule mji kwa hekima yake. Lakini hakuna aliyemkumbuka yule maskini.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi, kulionekana humo mtu maskini mwenye hekima, naye kwa hekima yake akauokoa mji ule lakini hata hivyo hapakuwa na mtu ye yote aliyemkumbuka yule mtu maskini.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Katika mji huo, alikuwapo maskini mmoja mwenye hekima, ambaye, kwa hekima yake aliuokoa mji huo. Lakini hakuna mtu aliyemkumbuka huyo maskini baadaye.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Katika mji huo kulikuwapo mtu mmoja maskini lakini mwenye hekima, naye akauokoa ule mji kwa hekima yake. Lakini hakuna aliyemkumbuka yule maskini.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Katika mji huo kulikuwepo mtu mmoja maskini lakini mwenye hekima, naye akauokoa ule mji kwa hekima yake. Lakini hakuna aliyemkumbuka yule maskini.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi, kulikuwemo na mtu maskini mwenye hekima, naye kwa hekima yake akauokoa mji ule lakini hata hivyo hapakuwa na mtu yeyote aliyemkumbuka yule mtu maskini.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Katika mji huo, alikuwapo maskini mmoja mwenye hekima, ambaye, kwa hekima yake aliuokoa mji huo. Lakini hakuna mtu aliyemkumbuka huyo maskini baadaye.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Basi, mle mjini akaonekana maskini mwenye werevu wa kweli, akauponya ule mji kwa huo werevu wake uliokuwa wa kweli; lakini baadaye hakuwako mtu aliyemkumbuka huyo maskini.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi, kulionekana humo mtu maskini mwenye hekima, naye kwa hekima yake akauokoa mji ule lakini hata hivyo hapakuwa na mtu ye yote aliyemkumbuka yule mtu maskini.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Katika muji ule, kulikuwa masikini mumoja mwenye hekima ambaye, kwa hekima yake, aliokoa muji ule. Lakini hakuna mutu aliyemukumbuka yule masikini kisha.