Ephesians 1:11 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Katika kuungana na Kristo, sisi tumerithishwa wokovu kama tulivyopangiwa kadiri ya azimio lake Mungu atekelezaye kila kitu kulingana na uamuzi na matakwa yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Katika Al-Masihi sisi nasi tumepata urithi, tukisha kuchaguliwa tangu awali sawasawa na kusudi la Mungu, yeye ambaye hufanya mambo yote kulingana na kusudi la mapenzi yake,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
na ndani yake sisi nasi tulifanywa urithi, huku tukichaguliwa tangu awali sawasawa na kusudi lake yeye, ambaye hufanya mambo yote kwa shauri la mapenzi yake.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Tulichaguliwa katika Kristo ili tuwe milki ya Mungu. Mungu alikwisha panga ili tuwe watu wake, kwa sababu ndivyo alivyotaka. Na ndiye ambaye hufanya kila kitu kifanyike kulingana na utashi na maamuzi yake.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kila kitu hufanywa kufuatana na mpango na uamuzi wa Mungu; naye Mungu ametuteua sisi tuwe watu wake kwa mapenzi yake katika kuungana na Kristo, kufuatana na azimio alilofanya tangu mwanzo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Katika kuungana na Kristo, sisi tumerithishwa wokovu kama tulivyopangiwa kadiri ya azimio lake Mungu atekelezaye kila kitu kulingana na uamuzi na matakwa yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Katika Kristo sisi nasi tumepata urithi, tukiisha kuchaguliwa sawasawa na kusudi la Mungu, yeye ambaye hufanya mambo yote kulingana na kusudi la mapenzi yake,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Katika Al-Masihi sisi nasi tumepata urithi, tukisha kuchaguliwa sawasawa na kusudi la Mungu, yeye ambaye hufanya mambo yote kulingana na kusudi la mapenzi yake,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
na ndani yake sisi nasi tulifanywa urithi, huku tukichaguliwa tangu awali sawasawa na kusudi lake yeye, ambaye hufanya mambo yote kwa shauri la mapenzi yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Katika kuungana na Kristo, sisi tumerithishwa wokovu kama tulivyopangiwa kadiri ya azimio lake Mungu atekelezaye kila kitu kulingana na uamuzi na matakwa yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yeye ndiye, ambaye tulipatiwa naye urithi wetu, tuliokatiwa kale na kuwekewa kale, maana yeye huyafanya yote, yawepo, kama ayatakavyo mwenyewe.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
na ndani yake sisi nasi tulifanywa urithi, huku tukichaguliwa tangu awali sawasawa na kusudi lake yeye, ambaye hufanya mambo yote kwa shauri la mapenzi yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mungu amefanya kila kitu kufuatana na kusudi na mapenzi yake. Yeye ametuchagua kwa njia ya kuungana kwetu na Kristo, kusudi tukuwe watu wake.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
ambae ndani yake sisi tumepata urithi, tukichaguliwa tangu awali kwa kusudi lake yeye afanyae yote kwa shauri la nia yake;