Ephesians 1:13 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nanyi pia watu wa mataifa mengine, mliusikia ujumbe wa kweli yaani Habari Njema iliyowaletea wokovu, mkamwamini Kristo; naye Mungu, ili kuonesha kuwa nyinyi ni wake, akawapiga mhuri kwa kuwapeni yule Roho Mtakatifu aliyetuahidia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ninyi pia mliingia ndani ya Al-Masihi mliposikia neno la kweli, Injili ya wokovu wenu. Baada ya kuamini, mlitiwa muhuri ndani yake, huyo Roho Mtakatifu wa Mungu mliyeahidiwa,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nanyi pia katika huyo mmekwisha kulisikia neno la kweli, habari njema za wokovu wenu; tena mmekwisha kumwamini yeye, na kutiwa muhuri na Roho yule wa ahadi aliye Mtakatifu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ndivyo ilivyo hata kwenu ninyi. Mliusikia ujumbe wa kweli, yaani Habari Njema kuhusu namna ambavyo Mungu anavyowaokoa. Mlipoisikia Habari Njema hiyo, mkamwamini Kristo. Na katika Kristo, Mungu aliwatia alama maalum kwa kuwapa Roho Mtakatifu aliyeahidi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Nanyi pia watu wa mataifa mengine, mliusikia ujumbe wa kweli yaani Habari Njema iliyowaletea wokovu, mkamwamini Kristo; naye Mungu, ili kuonyesha kuwa ninyi ni wake, akawapiga mhuri kwa kuwapeni yule Roho Mtakatifu aliyetuahidia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nanyi pia watu wa mataifa mengine, mliusikia ujumbe wa kweli yaani Habari Njema iliyowaletea wokovu, mkamwamini Kristo; naye Mungu, ili kuonesha kuwa nyinyi ni wake, akawapiga mhuri kwa kuwapeni yule Roho Mtakatifu aliyetuahidia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ninyi pia mliingia ndani ya Kristo mliposikia Neno la kweli, Injili ya wokovu wenu. Mkiisha kuamini, ndani yake mlitiwa muhuri, yaani, Roho Mtakatifu mliyeahidiwa,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ninyi pia mliingia ndani ya Al-Masihi mliposikia Neno la kweli, Injili ya wokovu wenu. Mkiisha kuamini, ndani yake mlitiwa muhuri, yaani, Roho wa Mwenyezi Mungu mliyeahidiwa,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nanyi pia katika huyo mmekwisha kulisikia neno la kweli, Habari Njema za wokovu wenu; tena mmekwisha kumwamini yeye, na kutiwa mhuri na Roho yule wa ahadi aliye Mtakatifu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nanyi pia watu wa mataifa mengine, mliusikia ujumbe wa kweli yaani Habari Njema iliyowaletea wokovu, mkamwamini Kristo; naye Mungu, ili kuonesha kuwa nyinyi ni wake, akawapiga mhuri kwa kuwapeni yule Roho Mtakatifu aliyetuahidia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nanyi mmelisikia Neno la kweli, ni ule Utume mwema wa wokovu wenu; napo hapo, mlipolitegemea, mlitiwa muhuri yake mlipompata Roho Mtakatifu, tuliyeagiwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nanyi pia katika huyo mmekwisha kulisikia neno la kweli, habari njema za wokovu wenu; tena mmekwisha kumwamini yeye, na kutiwa muhuri na Roho yule wa ahadi aliye Mtakatifu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ninyi vilevile, wakati muliposikia ujumbe wa kweli, maana yake Habari Njema iliyowaletea wokovu, mukamwamini Kristo. Naye Mungu akawapatia Roho Mutakatifu aliyeahidi kuwa kitambulisho cha kuhakikisha kwamba ninyi ni watu wake kabisa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
katika huyo na ninyi, mkiisha kulisikia neno la kweli, khabari njema ya wokofu wenu, katika huyo tena mkiisha kumwamini, mlitiwa muhuri na Roho yule Mtakatifu wa ahadi yake,