Ephesians 1:14 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Huyu Roho ni dhamana ya kupata yote yale Mungu aliyowaahidia watu wake, na jambo hili latuhakikishia kwamba Mungu atawakomboa kabisa wote walio wake. Tuusifu utukufu wake!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
yeye ambaye ni amana yetu ya kutuhakikishia urithi wetu hadi ukombozi wa wale walio milki ya Mungu, kwa sifa ya utukufu wake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndiye aliye arabuni ya urithi wetu, ili kuleta ukombozi wa milki yake, kuwa sifa ya utukufu wake.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Roho ni malipo ya kwanza yanayothibitisha kuwa Mungu atawapa watu wake kila kitu alichonacho kwa ajili yao. Sisi sote tutaufurahia uhuru kamili uliowekwa tayari kwa ajili ya walio wake. Na hili litamletea Mungu sifa katika utukufu wake wote.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Huyu Roho ni dhamana ya kurithi yote yale Mungu aliyowaahidia watu wake, na jambo hili latuhakikishia kwamba Mungu atawakomboa kabisa wote walio wake. Tuusifu utukufu wake!
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Huyu Roho ni dhamana ya kupata yote yale Mungu aliyowaahidia watu wake, na jambo hili latuhakikishia kwamba Mungu atawakomboa kabisa wote walio wake. Tuusifu utukufu wake!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
yeye ambaye ni amana yetu akituhakikishia urithi wetu hadi ukombozi wa wale walio milki ya Mungu kwa sifa ya utukufu wake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
yeye ambaye ni amana yetu akituhakikishia urithi wetu hadi ukombozi wa wale walio milki ya Mungu kwa sifa ya utukufu wake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndiye aliye arabuni ya urithi wetu, ili kuleta ukombozi wa milki yake, kuwa sifa ya utukufu wake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Huyu Roho ni dhamana ya kupata yote yale Mungu aliyowaahidia watu wake, na jambo hili latuhakikishia kwamba Mungu atawakomboa kabisa wote walio wake. Tuusifu utukufu wake!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Huyu ni rehani ya urithi wetu, tujue: tumekombolewa, tu watu wake, utukufu wake upate wenye kuusifu.*
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndiye aliye arabuni ya urithi wetu, ili kuleta ukombozi wa milki yake, kuwa sifa ya utukufu wake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yule Roho ni rehani ya urizi aliowawekea watu wake. Na jambo hili linahakikisha kwamba Mungu atakomboa kabisa wote wanaokuwa wake. Tumusifu kwa ajili ya utukufu wake.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
aliye arabuni ya urithi wetu, hatta ukombozi wa milki yake Mungu, kwa sifa ya utukufu wake.