Ephesians 1:21 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Huko, Kristo anatawala juu ya kila tawala, mamlaka, enzi na ukuu; anatawala juu ya kila cheo kiwezacho kutajwa katika ulimwengu huu na katika ulimwengu ujao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
juu sana kuliko falme zote na mamlaka, enzi na milki, na juu ya kila jina litajwalo, si katika ulimwengu huu tu, bali katika ule ujao pia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
juu sana kuliko ufalme wote, na mamlaka, na nguvu, na usultani, na kila jina litajwalo, wala si ulimwenguni humu tu, bali katika ule ujao pia;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Amemweka Kristo juu ya watawala wote, mamlaka zote, nguvu zote na wafalme wote. Amempa mamlaka juu ya kila kitu chenye nguvu katika ulimwengu huu na ujao.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Huko, Kristo anatawala juu ya kila tawala, mamlaka, enzi na ukuu; anatawala juu ya kila cheo kiwezacho kutajwa katika ulimwengu huu na katika ulimwengu ujao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Huko, Kristo anatawala juu ya kila tawala, mamlaka, enzi na ukuu; anatawala juu ya kila cheo kiwezacho kutajwa katika ulimwengu huu na katika ulimwengu ujao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
juu sana kuliko falme zote na mamlaka, enzi na milki na juu ya kila jina litajwalo, si katika ulimwengu huu tu, bali na katika ule ujao pia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
juu sana kuliko falme zote na mamlaka, enzi na milki, na juu ya kila jina litajwalo, si katika ulimwengu huu tu, bali katika ule ujao pia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
juu sana kuliko ufalme wote, na mamlaka, na nguvu, na utawala, na kila jina litajwalo, wala si ulimwenguni humu tu, bali katika ule ujao pia;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Huko, Kristo anatawala juu ya kila tawala, mamlaka, enzi na ukuu; anatawala juu ya kila cheo kiwezacho kutajwa katika ulimwengu huu na katika ulimwengu ujao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
na kumpa cheo kuupita ukubwa na ufalme na uwezo na ubwana wote na kuyapita majina yo yote yatakayotajwa siku hizi, nazo siku zote zitakazokuja.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
juu sana kuliko ufalme wote, na mamlaka, na nguvu, na usultani, na kila jina litajwalo, wala si ulimwenguni humu tu, bali katika ule ujao pia;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na kule anatawala juu ya wakubwa wote, wenye mamlaka wote, wenye uwezo wote na wasultani wote na juu ya kila cheo kinachoweza kuwa katika dunia hii na katika dunia itakayokuja.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
juu sana kuliko ufalme wote, na mamlaka, na nguvu, na usultani, na killa jina litajwalo, si ulimwenguni humu tu, bali katika ule ujao nao;