Ephesians 1:5 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mungu alikuwa ameazimia tangu zamani kutuleta kwake kama watoto wake kwa njia ya Yesu Kristo. Ndivyo alivyopenda na kunuia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
alitangulia kutuchagua tuwe wanawe kupitia kwa Isa Al-Masihi kwa furaha na mapenzi yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa kuwa alitangulia kutuchagua, ili tufanywe wanawe kwa njia ya Yesu Kristo, sawasawa na uradhi wa mapenzi yake.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Aliamua tangu mwanzo kutufanya kuwa watoto wake kupitia Yesu Kristo. Hivi ndivyo Mungu alivyotaka na ilimpendeza yeye kufanya hivyo.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mungu alikuwa ameazimia tangu zamani kutuleta kwake kama watoto wake kwa njia ya Yesu Kristo. Ndivyo alivyopenda na kunuia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mungu alikuwa ameazimia tangu zamani kutuleta kwake kama watoto wake kwa njia ya Yesu Kristo. Ndivyo alivyopenda na kunuia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa upendo alitangulia kutuchagua tuwe wanawe kwa njia ya Yesu Kristo kwa furaha yake na mapenzi yake mwenyewe.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
alitangulia kutuchagua tuwe wanawe kwa njia ya Isa Al-Masihi kwa furaha yake na mapenzi yake mwenyewe.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa kuwa alitangulia kutuchagua, ili tufanywe wanawe kwa njia ya Yesu Kristo, kulingana na radhi ya mapenzi yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mungu alikuwa ameazimia tangu zamani kutuleta kwake kama watoto wake kwa njia ya Yesu Kristo. Ndivyo alivyopenda na kunuia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hivyo, anavyotupenda, alitutenga kale, tupokelewe kuwa wana wake mwenyewe tukimfuata Yesu Kristo; ndiyo yaliyompendeza, akayataka, yawepo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa kuwa alitangulia kutuchagua, ili tufanywe wanawe kwa njia ya Yesu Kristo, sawasawa na uradhi wa mapenzi yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mungu amekusudia tangu zamani kutukubali sisi kuwa watoto wake kwa njia ya Yesu Kristo. Alifanya vile kufuatana na mapenzi yake.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa kuwa ametuchagua tangu zamani illi tufanywe waua wake yeye kwa njia ya Yesu Kristo, kwa mapenzi ya nia yake,