Ephesians 2:11 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nyinyi mlio kwa asili watu wa mataifa mengine — mnaoitwa, “Wasiotahiriwa” na Wayahudi ambao hujiita, “Waliotahiriwa,” (kwa sababu ya kile wanachoifanyia miili yao) — kumbukeni mlivyokuwa zamani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo kumbukeni kwamba hapo awali ninyi ambao ni watu wa Mataifa kwa kuzaliwa na kuitwa “wasiotahiriwa” na wale wanaojiita “waliotahiriwa” (yaani tohara ifanyikayo katika mwili kwa mikono ya wanadamu),
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa ajili ya hayo kumbukeni ya kwamba zamani ninyi, mlio watu wa Mataifa kwa jinsi ya mwili, mnaoitwa Wasiotahiriwa na wale wanaoitwa Waliotahiriwa, yaani, tohara ya mwilini iliyofanyika kwa mikono;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hamkuzaliwa mkiwa Wayahudi. Ninyi ni watu ambao Wayahudi huwaita “Wasiotahiriwa”, na wao wakijiita “Waliotahiriwa” (Tohara yao ni ile inayofanyika kwenye miili yao kwa mikono ya binadamu.)
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Ninyi mlio kwa asili watu wa mataifa mengine—mnaoitwa, “wasiotahiriwa” na Wayahudi ambao hujiita, “Waliotahiriwa,” (kwa sababu ya kile wanachoifanyia miili yao) —kumbukeni mlivyokuwa zamani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nyinyi mlio kwa asili watu wa mataifa mengine — mnaoitwa, “Wasiotahiriwa” na Wayahudi ambao hujiita, “Waliotahiriwa,” (kwa sababu ya kile wanachoifanyia miili yao) — kumbukeni mlivyokuwa zamani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo kumbukeni kwamba ninyi ambao hapo awali mlikuwa watu Mataifa kwa kuzaliwa na kuitwa “wasiotahiriwa” na wale wanaojiita “waliotahiriwa” (yaani tohara ifanyikayo katika mwili kwa mikono ya wanadamu),
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo kumbukeni kwamba ninyi ambao hapo awali mlikuwa watu wa Mataifa kwa kuzaliwa na kuitwa “wasiotahiriwa” na wale wanaojiita “waliotahiriwa” (yaani tohara ifanyikayo katika mwili kwa mikono ya wanadamu),
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa ajili ya hayo kumbukeni ya kwamba zamani ninyi, mlio watu wa Mataifa kwa jinsi ya mwili, mnaoitwa Wasiotahiriwa na wale wanaoitwa Waliotahiriwa, yaani, tohara ya mwilini iliyofanyika kwa mikono;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nyinyi mlio kwa asili watu wa mataifa mengine – mnaoitwa, “Wasiotahiriwa” na Wayahudi ambao hujiita, “Waliotahiriwa,” (kwa sababu ya kile wanachoifanyia miili yao) – kumbukeni mlivyokuwa zamani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo yakumbukeni: kale mlikuwa wamizimu kwa hivyo, miili yenu ilivyo; mkaitwa mapumbavu nao wale waliojiita makungwi, kwa sababu walikuwa wametahiriwa na mikono ya watu miilini mwao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa ajili ya hayo kumbukeni ya kwamba zamani ninyi, mlio watu wa Mataifa kwa jinsi ya mwili, mnaoitwa Wasiotahiriwa na wale wanaoitwa Waliotahiriwa, yaani, tohara ya mwilini iliyofanyika kwa mikono;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi mukumbuke namna mulivyokuwa zamani ninyi munaokuwa kwa kizalikio watu wa mataifa mengine. Wayuda wanawaita ninyi watu wasiotahiriwa, lakini wao wanajiita wenye kutahiriwa kwa sababu ya kitambulisho cha kutahiriwa na watu katika miili yao.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa ajili ya hayo kumbukeni kwamba zamani, ninyi mlio watu wa mataifa kwa jinsi ya mwili, mnaoitwa jina lenu wasiotahiriwra na wale wanaoitwa jina lao waliotahiriwa, yaani tohara ya mwili kwa mikono: