Ephesians 2:12 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakati ule nyinyi mlikuwa bila Kristo; mlikuwa nje ya jamii ya Israeli; mlikuwa wageni na hamkuwa na sehemu katika yale maagano aliyoahidi Mungu. Mlikuwa bila matumaini na kama watu wasiomjua Mungu hapa duniani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
kumbukeni kwamba wakati ule mlikuwa mbali na Al-Masihi, mkiwa mmetengwa kutoka jumuiya ya Israeli, na mkiwa wageni katika yale maagano ya ahadi, nanyi hamkuwa na tumaini wala Mungu duniani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
kwamba zamani zile mlikuwa hamna Kristo, mmefarakana na jamii ya Israeli, wageni wasio wa maagano ya ahadi ile. Mlikuwa hamna tumaini, hamna Mungu duniani.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kumbukeni ya kwamba zamani hamkuwa na Kristo. Hamkuwa raia wa Israeli na hamkujua kuhusu mapatano ya maagano ambayo Mungu aliyaweka kwa watu wake. Hamkuwa na tumaini na hamkumjua Mungu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Wakati ule ninyi mlikuwa bila Kristo; mlikuwa nje ya jamii ya Israeli; mlikuwa wageni na hamkuwa na sehemu yoyote katika lile agano la zile ahadi. Mlikuwa bila matumaini Mungu hapa duniani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakati ule nyinyi mlikuwa bila Kristo; mlikuwa nje ya jamii ya Israeli; mlikuwa wageni na hamkuwa na sehemu katika yale maagano aliyoahidi Mungu. Mlikuwa bila matumaini na kama watu wasiomjua Mungu hapa duniani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
kumbukeni kwamba wakati ule mlikuwa hamna Kristo, mkiwa mmtengwa kutoka katika jumuiya ya watu wa Mungu, yaani, Israeli mkiwa wageni katika yale maagano ya ahadi, mliishi duniani mkiwa hamna tumaini wala Mungu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
kumbukeni kwamba wakati ule mlikuwa mbali na Al-Masihi, mkiwa mmetengwa kutoka jumuiya ya Israeli, na mkiwa wageni katika yale maagano ya ahadi, nanyi mkiwa hamna tumaini wala Mwenyezi Mungu duniani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
kwamba zamani zile mlikuwa hamna Kristo, mmefarakana na jamii ya Israeli, wageni wasio wa maagano ya ahadi ile. Mlikuwa hamna tumaini, hamna Mungu duniani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakati ule nyinyi mlikuwa bila Kristo; mlikuwa nje ya jamii ya Israeli; mlikuwa wageni na hamkuwa na sehemu katika yale maagano aliyoahidi Mungu. Mlikuwa bila matumaini na kama watu wasiomjua Mungu hapa duniani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kumbukeni: siku zile mlikuwa hamnaye Kristo, tena mlikuwa mmekatazwa kuwa wenyeji kwao Waisiraeli, mkawa wageni, msiyajue maagano, waliyoagiwa kuyapata. Mlikuwa hamnacho kingojeo, wala hamnaye Mungu huku ulimwenguni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
kwamba zamani zile mlikuwa hamna Kristo, mmefarakana na jamii ya Israeli, wageni wasio wa maagano ya ahadi ile. Mlikuwa hamna tumaini, hamna Mungu duniani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa wakati ule mulikuwa mumetengwa mbali na Kristo. Hamukukuwa kati ya watu waliochaguliwa na Mungu, mulikuwa wageni kati yao. Ninyi hamukukuwa na pato lolote katika agano zile Mungu alizotoa katika ahadi yake kwa watu wake. Muliishi katika dunia pasipo tumaini wala kumujua Mungu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
kwamba zamani zile mlikuwa hamna Kristo, mmefarakana na jamii ya Israeli, wageni, wasio wa maagano ya ahadi; mlikuwa hamna tumaini, hamna Mungu duniani.