Ephesians 2:16 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa mwili wake, Kristo aliuangamiza uadui wao; kwa msalaba wake aliziunganisha jamii hizo kuwa moja na kuzipatanisha na Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
naye katika mwili huu mmoja awapatanishe wote wawili na Mungu kupitia msalaba, ili kwa huo msalaba akaangamiza uadui wao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akawapatanisha wote wawili na Mungu katika mwili mmoja, kwa njia ya msalaba, akiisha kuufisha ule uadui kwa huo msalaba.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kupitia msalaba Kristo alisitisha uhasama kati ya makundi mawili. Na baada ya makundi haya kuwa mwili mmoja, alitaka kuwapatanisha wote tena kwa Mungu. Alifanya hivi kwa kifo chake msalabani.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kwa mwili wake, Kristo aliuangamiza uadui wao; kwa msalaba wake aliziunganisha jamii hizo kuwa moja na kuzipatanisha na Mungu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa mwili wake, Kristo aliuangamiza uadui wao; kwa msalaba wake aliziunganisha jamii hizo kuwa moja na kuzipatanisha na Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
naye katika mwili huu mmoja awapatanishe wote wawili na Mungu kwa kupitia msalaba, ambao kwa huo aliangamiza uadui wao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
naye katika mwili huu mmoja awapatanishe wote wawili na Mwenyezi Mungu kupitia msalaba, ili kwa huo msalaba akaangamiza uadui wao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akawapatanisha wote wawili na Mungu katika mwili mmoja, kwa njia ya msalaba, akiisha kuumaliza ule uadui kwa huo msalaba.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa mwili wake, Kristo aliuangamiza uadui wao; kwa msalaba wake aliziunganisha jamii hizo kuwa moja na kuzipatanisha na Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
akawa kole yao wote wawili alipomlipa Mungu madeni yao yeye mmoja mwilini mwake, alipowambwa msalabani; huko ndiko, alikoyaua yale machukivu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akawapatanisha wote wawili na Mungu katika mwili mmoja, kwa njia ya msalaba, akiisha kuufisha ule uadui kwa huo msalaba.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kristo alivunja uadui kwa njia ya kufa kwake juu ya musalaba, akaunganisha watu wa makabila haya mawili kuwa moja na kuwapatanisha na Mungu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
na kuwapatanisha wote wawili na Mungu katika mwili mmoja, kwa msalaba, akiisha kuuua ule uadui kwa huo msalaba;