Ephesians 2:19 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, nyinyi si wageni tena, wala si watu wa nje. Nyinyi ni raia pamoja na watu wa Mungu, na ni watu wa jamaa ya Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivyo basi, ninyi sasa si wageni tena na wapitaji, bali mmekuwa wenyeji pamoja na watakatifu na pia jamaa wa nyumbani mwake Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi tangu sasa ninyi si wageni wala wapitaji, bali ninyi ni wenyeji pamoja na watakatifu, watu wa nyumbani mwake Mungu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hivyo ninyi msio Wayahudi si wageni wala wahamiaji, lakini ninyi ni raia pamoja na watakatifu wa Mungu. Ninyi ni wa familia ya Mungu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, ninyi si wageni tena, wala si watu wa nje; ninyi ni raia pamoja na watu wa Mungu, na ni watu wa jamaa ya Mungu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, nyinyi si wageni tena, wala si watu wa nje. Nyinyi ni raia pamoja na watu wa Mungu, na ni watu wa jamaa ya Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivyo basi, ninyi sasa si wageni tena wala wapitaji, bali mmekuwa wenyeji pamoja na watakatifu na pia jamaa wa nyumbani mwake Mungu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivyo basi, ninyi sasa si wageni tena wala wapitaji, bali mmekuwa wenyeji pamoja na watakatifu, na pia jamaa wa nyumbani mwake Mwenyezi Mungu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi tangu sasa ninyi si wageni wala wapitaji, bali ninyi ni wenyeji pamoja na watakatifu, watu wa nyumbani mwake Mungu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, nyinyi si wageni tena, wala si watu wa nje. Nyinyi ni raia pamoja na watu wa Mungu, na ni watu wa jamaa ya Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
*Kwa hiyo sasa ham wageni tena, wala wenye kukaa kando, ila m wenyeji pamoja nao watakatifu, tena m wa nyumbani mwake Mungu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi tangu sasa ninyi si wageni wala wapitaji, bali ninyi ni wenyeji pamoja na watakatifu, watu wa nyumbani mwake Mungu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi sasa, ninyi watu wa mataifa mengine si wageni tena wala wapangaji. Lakini sasa mumekuwa wanainchi pamoja na watu wa Mungu na tena mumekuwa watu wa jamaa la Mungu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi tangu sasa ninyi si wapitaji wala wageni, bali ninyi ni wenyeji pamoja na watakatifu, watu wa nyumba ya Mungu,