Ephesians 2:3 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Na hata sisi sote tulikuwa kama wao; tuliishi kufuatana na tamaa zetu za kidunia na kufanya tu mambo yale yaliyoipendeza miili na akili zetu. Kidunia, sisi kama vile pia wao, tulistahili ghadhabu ya Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Sisi sote pia tuliishi katikati yao hapo zamani, tukitimiza tamaa za asili yetu ya dhambi na kufuata tamaa zake na mawazo yake. Nasi kwa asili tulistahili ghadhabu, kama watu wengine wote.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
ambao zamani, sisi sote nasi tulienenda kati yao, katika tamaa za miili yetu, tulipoyatimiza mapenzi ya mwili na ya nia, tukawa kwa tabia yetu watoto wa hasira kama na hao wengine.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Tuliishi hivyo zamani, tukijaribu kuzifurahisha tamaa zetu za mwili. Tulitenda mambo ambayo miili na akili zetu zilitaka. Kama ilivyo kwa kila mtu ulimwenguni, tulistahili kuteseka kutokana na hasira ya Mungu kwa sababu ya jinsi tulivyokuwa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Na hata sisi sote tulikuwa kama wao; tuliishi kufuatana na tamaa zetu za kidunia na kufanya tu mambo yale yaliyoipendeza miili na akili zetu. Kidunia, sisi kama vile pia wao, tulistahili ghadhabu ya Mungu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Na hata sisi sote tulikuwa kama wao; tuliishi kufuatana na tamaa zetu za kidunia na kufanya tu mambo yale yaliyoipendeza miili na akili zetu. Kidunia, sisi kama vile pia wao, tulistahili ghadhabu ya Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Sisi sote pia tuliishi katikati yao hapo zamani, tukitimiza tamaa za asili yetu ya dhambi na kufuata tamaa zake na mawazo yake. Nasi kwa asili tulikuwa wana wa ghadhabu, kama mtu mwingine ye yote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Sisi sote pia tuliishi katikati yao hapo zamani, tukitimiza tamaa za asili yetu ya dhambi na kufuata tamaa zake na mawazo yake. Nasi kwa asili tulikuwa wana wa ghadhabu, kama mtu mwingine yeyote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
ambao zamani, sisi sote nasi tulienda kati yao, katika tamaa za miili yetu, tulipoyatimiza mapenzi ya mwili na ya nia, tukawa kwa tabia yetu watoto wa hasira, kama wengineo wote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Na hata sisi sote tulikuwa kama wao; tuliishi kufuatana na tamaa zetu za kidunia na kufanya tu mambo yale yaliyoipendeza miili na akili zetu. Kidunia, sisi kama vile pia wao, tulistahili ghadhabu ya Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nasi sote kale tulikuwa wenzao tulipoendelea na kuzifuata tamaa za miili yetu na kuyafanya, miili na mioyo yetu iliyoyataka, nasi kwa hivyo, tulivyokuwa hapo, tulikuwa wana waliomkasirisha kama wale wengine.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
ambao zamani, sisi sote nasi tulienenda kati yao, katika tamaa za miili yetu, tulipoyatimiza mapenzi ya mwili na ya nia, tukawa kwa tabia yetu watoto wa hasira kama na hao wengine.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Zamani, sisi wote vilevile tulikuwa kama wao. Tuliishi kufuatana na tamaa zetu za kimwili na kutenda kufuatana na mapenzi ya mwili na roho zetu. Kwa sababu ya hali yetu ya kimwili, hatungeponyoka kasirani ya Mungu kama wengine.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
ambazo sisi nasi sote tuliziendea, hapo zamani, katika tamaa za mwili wetu, tukiyatimiza mapenzi ya mwili wetu na ya nia zetu, tukawa kwa tabia yetu watoto wa ghadhabu kama na hao wengine.